VIDEO: Magufuli awajibu wanaosema hampendi Gambo

VIDEO: Magufuli awajibu wanaosema hampendi Gambo

Muktasari:

Magufuli awajibu wanaosema hampendi mgombea ubunge wa CCM Arusha mjini, Mrisho Gambo akisisitiza kuwa alimpeleka Arusha kwenda kuukomboa mjini huo

Dar es Salaam. Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli ameeleza kushangazwa kwake na watu wanaomsema kuwa hampendi mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya chama hicho, Mrisho Gambo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Arusha leo Ijumaa Oktoba 23, 2020, Magufuli amesema Gambo ndio atakayekwenda kuikomboa Arusha.

Magufuli amesema alipata wakati mgumu  kupeleka maendeleo Arusha kutokana mji huo kuongozwa na upinzani hivyo alimpeleka Gambo kwenda kufanya mabadiliko.

“Nilipata wakati mgumu sana Arusha hadi nikaamua kumteua Gambo ili awe ananipa taarifa za hapa. Nilimwambia Gambo nenda kafanye kazi kama mkuu wa mkoa na mbunge wa Arusha mjini na amefanya kazi nzuri mno.”

“Sikumfukuza ukuu wa mkoa wala aliyekuwa mkuu wa wilaya wa hapa. Gambo aliniomba kwa kuniambia kuwa ameiona Arusha inakwenda vibaya ninaomba nikaikomboe nikamwambia nenda na Mungu akusaidie. Ninawashangaa watu wanaposimama kwenye majukwaa na kusema Gambo simpendi, ningekuwa simpendi ningerudisha jina lake aje kugombea?” amehoji Magufuli.