Vigogo wanne wa bandari waburuzwa mahakamani

Muktasari:

  • Waliokuwa wafanyakazi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85 milioni sawa na Sh4.2 bilioni.

Dar es Salaam. Waliokuwa wafanyakazi waandamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka matatu, likiwamo la kuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Dola za Marekani 1.85 milioni sawa na Sh4.2 bilioni.

Washtakiwa hao ni aliyekuwa Ofisa Rasilimali watu, Peter Gawile (58), aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Manununuzi, Casmily Lujegi (65).

Wengine ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Manununuzi, Mashaka Kisanta (59) na Kilian Chale (51) ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Wamefikishwa mahakamani hapo leo, Juni 30, 2022 na kusomewa mashtaka na wakili wa Serikali, Timotheo Mmari akisaidiana na Mosia Kaima, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemalira.