Viongozi, wananchi wawasili miaka 58 Mapinduzi Zanzibar

Maadhimisho miaka 58 Mapinduzi Zanzibar

Muktasari:

Leo ikiwa ni kilele cha sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar, wananchi na viongozi mbalimbali wameshaingia katika uwanja wa Amaan yanapofanyika maadhimisho hayo.

Unguja. Leo ikiwa ni kilele cha sherehe za miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar, wananchi na viongozi mbalimbali wameshaingia katika uwanja wa Amaan yanapofanyika maadhimisho hayo.

Baadhi ya viongozi ambao wamewasili ni pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda na Fredrick Sumaye, Makamu wa Rais mstaafu Dk Gharib Bilali, Makamu wa kwanza wa Rais Othman Masoud na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama huku viongozi wengine wakiendelea kuwasili.

Kwa mujibu wa ratiba, viongozi ambao wanasubiriwa ni pamoja na Rais wa Tanzania, Samaia Suluhu Hassan pamaoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ambaye ndiye mgeni rasmi katika sherehe hizo.