Waathirika 973 biashara ya usafirishaji wa binadamu waokolewa

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene amesema jumla ya waathirika 973 wa biashara ya usafirishaji wa binadamu waliokolewa ndani na nje ya nchi ambapo kati ya hao 37 waliokolewa nje ya Tanzania.

Dodoma. Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene amesema jumla ya waathirika 973 wa biashara ya usafirishaji wa binadamu waliokolewa ndani na nje ya nchi ambapo kati ya hao 37 waliokolewa nje ya Tanzania.

Simbachawene ameyasema hayo leo Ijumaa Novemba 26, 2021 wakati akizungumzia mafanikio ya wizara hiyo katika miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara.

Amesema kufikia Novemba 2021 kesi 75 zilizohusisha usafirishaji wa biashara haramu ya watu katika mahakama mbalimbali nchini.

Amesema jumla ya wahalifu 63 wamehukumiwa kutumikia vifungo magerezani na kwamba Serikali imeokoa na kusaidia wahanga 973 waliokuwa wakitumikishwa mitaani na nje ya nchi.

Amesema 936 kati ya wahanga hao waliokolewa nchini na kwamba 857 ni Watanzania 20 (Burundi), 25 (Nepal), 30 (India), mmoja (Msumbiji) na mmoja (Afrika Kusini).

Amesema wahanga 37 waliokolewa kutoka nje ya nchi hususan Thailand (7), India (4), Oman (3), Yemen (1), Kenya (14) Malasia (2), Uganda (1) na Iraq (5).