Wabunge 19 Viti Maalum Chadema hawa hapa

Tuesday November 24 2020
viti maalum pic
By Ephrahim Bahemu

Dar es Salaam. Wabunge 19 wa Viti Maalum Chadema wameapishwa na Spika wa Bunge jijini  Dodoma leo Jumanne Novemba 24, 2020 huku wengi wakiwa ni waliokuwa wabunge katika Bunge lililopita.

Awali kabla ya kuwaapisha Spika Job Ndugai alianza kwa kunukuu vifungu vya katiba na kusema Chadema kilifikia idadi ya kura zinazotosha kuwapa wabunge wa Viti Maalum na Novemba 20, 2020 alipokea barua kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yenye maelezo juu ya wabunge walioteuliwa kwa mwaka 2020.

Walioapishwa ni HalIma Mdee, Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo, Asia Mohammed.

Wengine ni Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza.


Advertisement