Wabunge CCM Arusha kumpitisha Dk Tulia

Muktasari:

  • Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Arusha, wameipongeza Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza jina la Dk Tulia Ackson kuwa mgombea pekee wa nafasi ya uspika wa Bunge.

Arusha. Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Arusha, wameipongeza Kamati Kuu ya chama hicho kutangaza jina la Dk Tulia Ackson kuwa mgombea pekee wa nafasi ya uspika wa Bunge.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Taifa ,William Sarakikya leo Ijumaa Januari 21, 2022 amesema Kamati hiyo imefanya jambo jema la kumpitisha Dk Tulia kuwa mgombea pekee katika nafasi ya uspika.

Sarakikya amesema wanashauri apewe kura zote na wabunge kwani ana sifa, uwezo, uzoefu na amedhihirisha uwezo wa kumudu changamoto za kuliongoza Bunge kwa weledi, umahiri na ufanisi.

“Tunaimani kubwa kwa Dk Tulia anauwezo wa kushirikiana na wabunge kuishauri Serikali jinsi ya kukabiliana na changamoto” amesema.