Wabunge vijana wanena haya kuhusu mimba shuleni

Tuesday June 28 2022
bungeeepiic
By Mainda Mhando

Dodoma.  Katika kuhakikisha mimba shuleni zinakomeshwa, wabunge vijana wameiomba serikali kutenga sehemu za siri kwa ajili ya kuchukua kondomu na dawa za uzazi wa mpango.

Ombi hilo limekuja kufuatia mioundombinu ya vituo vya afya na ushauri wa afya ya uzazi kutokuwa rafiki kwani hakuna faragha kwa watumiaji.

Maombi hayo yametolewa leo Jumatatu Juni 27, 2022 kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii na chama cha wazazi na malezi bora Tanzania (UMATI).

Akizungumza kwa niaba ya vijana, Tausi  Libiga amesema kwa asili ya jamii iliyopo, huwa ngumu kwa vijana wengi kwenda kwenye vituo hivyo kuchukua zana za uzazi wa mpango.

Advertisement