Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wadau wa utalii kunogesha sherehe za AU kilele cha mlima Kilimanjaro

Moshi. Wadau wa utalii nchini wamesema watatumia  mlima Kilimanjaro kama jukwaa la kuunganisha vijana wa Afrika wenye ndoto na maono  tofauti kupitia sanaa ya uchoraji katika kueneza ujumbe wa Afrika unaosema 'Afrika tunayoitaka' ifikapo 2063 ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya siku ya Umoja wa Afrika(AU) ambayo huadhimishwa ifikapo Mei 25, kila mwaka.

Akizungumza leo Aprili 29, Mkurugenzi wa kampuni ya Origin Trails ambayo inajihusisha na shughuli za utalii, Emannuel Mota amesema siku ya Umoja wa Afrika(AU)  watatumia sanaa ya uchoraji  kupitia picha kwa sababu sanaa inaeleza zaidi kuliko maneno mtu ambayo anaweza kusema lakini katika lugha ambayo kila mtu anaweza kuitafsiri kwa aina yake.

Amesema kama ni mchoraji siku hiyo atachora picha kuhusu Afrika anayoitaka, kama ni mwimbaji ataimba wimbo wa Afrika anayoitaka na Mwandishi pia ataandika Afrika anayoitaka na kwamba mawazo yao yatachorwa kupitia wataalam mbalimbali watakaoshiriki siku hiyo.

"Program hii tutakayoitumia itasaidia kuutangaza mlima Kilimanjaro kama kivutio cha utalii kwa wingi kwa sababu Waafrika nafikiri sio wengi wanaopanda mlima Kilimanjaro ni wachache, na wanaopanda ni kutoka Mabara  mengine," amesema Mota

"Tutautangaza mlima huu kwa nchi zote za Afrika kwa vijana na wote wenye maono kuhusu Afrika tunayoitaka jukwaa ambalo linajumuisha kila mtu, mtu anaweza kuchangia kueleza Afrika anayoitaka, kama ni mchoraji basi atachora picha kuhusu Afrika anayoitaka, mwimbaji ataimba wimbo wa Afrika anayoitaka, Mwandishi anaweza kuandika Afrika unayoitaka, lakini zote hizi zitapelekwa kwa wachoraji ili wachore mawazo yetu ambayo hatuwezi kuchora kama wao,"

Amesema baada ya kuchorwa picha hizo na kuwekwa kwenye vitambaa, watazipeleka moja kwa moja katika  kilele cha mlima Kilimanjaro lengo ikiwa ni kuutangaza mlima Kilimanjaro katika Bara la Afrika.

"Katika kila kituo wachoraji wataendelea kuchora mawazo ya  Afrika wanayoitaka, mawazo haya na picha hizi zitapelekwa moja kwa moja mpaka juu ya kilele cha mlima Kilimanjaro, tutatumia sanaa na sanaa hii itakayowekwa kwenye vitambaa itaunganishwa na kila nchi itatengeneza ukubwa wa kilomita moja ya picha,"

"Picha hizi zitaunganishwa mpaka zitafika kila nchi kilomita moja moja kwa hiyo tutakuwa na kimomita 55 za picha pamoja na kilomita moja ya Waafrika ambao wanaishi nje ya bara la Afrika, hii ni ndoto na maono ya kila Mwafrika ambayo tunataka tuyalete pamoja na tutumie mlima Kilimanjaro kama jukwaa la kupaza sauti za Waafrika kuhusu Afrika wanayoitaka,"

Mkurugenzi wa The African Great Art Banner (GAAB), Munyaradzi Muzenda, amewataka vijana wa Afrika kutumia fursa hiyo kuonyesha vipaji mbalimbali walivyonavyo kama sehemu ya ajira.

"Tukio hili pia ni fursa kwa wachoraji maana anaweza kutengeneza ajira nyingi za kudumu wakati tukielekea katika siku hii muhimu kwa Waafrika, hii ni fursa kubwa sana ya  ajira lakini watu hawaoni hilo zaidi watu wengi wamekuwa wakisubiri tuu kuambiwa,"

Naye Ofisa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Vitus Mgaya, amesema watahakikisha wanaunga mkono jitihada hizo zinazofanywa na wadau wa utalii hapa nchini ili azma yao hiyo  iweze kutimia.

"Sisi kama Kinapa tupo hapa kwa ajili ya kuwaunga mkono maana kitu hiki ni muhimu kwa nchi za Afrika na ujumbe utaokaobebwa ni wa Afrika kueleza kitu wanachokitaka ambayo ni agenda ya Umoja wa Afrika (AU)  2063.

"Tutahakikisha program hii inaenda sawa kuanzia mwanzo maana ni agenda itakayo kuwepo kwa maiaka 40 sasa na  itasiaida Waafrika na dunia nzima kuujua mlima Kilimanjaro na wengine kuweza kuvutiwa kuja kuupanda mlima wetu,"