Wafanyabiashara Kiteto wabadili changamoto kunyauka mazao kuwa fursa

Baadhi ya wafanya biashara wa mahindi wakihesabiana mahindi ambayo yametoka Wilaya ya Kilindi kwa ajili ya kuuzwa Kiteto. Picha Mohamed Hamad Kiteto

Muktasari:

  • Waagiza bidhaa mbalimbali yakiwemo mahindi mabichi, mchele, viazi na maharage nje ya wilaya na nikoa ya jirani kunusuru wananchi

Kiteto. Changamoto ya mazao kunyauka kutokana na uchache wa mvua mwaka huu wilayani Kiteto mkoani Manyara kutokana na mabadiliko ya tabianchi, wafanyabiashara wamegeukia kununua mazao mbalimbali kwa wilaya za jirani  na mikoa ya jirani ikiwemo Tanga wamegeuza changamoto hiyo kuwa fursa kwa.

Wakizungumza na mwananchi Digital, baadhi ya wafanyabiashara hao leo Machi 23, 2023 mjini Kibaya wamesema wamebadili changamoto hiyo ya mahindi kunyauka kuwa fursa.

Wilaya ya Kiteto imezoeleka ndio inalisha maeneo mengi chakula hapa nchini lakini safari hii imekuwa ni tofauti, wananchi wanahitaji msaada wa chakula cha bei nafuu kutoka serikalini.

"Hivi sasa wilaya na mikoa ya jirani ndio wanatusaidia kupata bidhaa mbalimbali kama vile mahindi mabichi viazi, maharage na michele kutoka Wilaya ya Kilindi Tanga na maeneo mengine, na hii ni baada ya kubadili changamoto ya kunyauka mazao kuwa fursa," alisema Seif Athumani Haji Muuza mahindi mabichi Kiteto.

"Mahindi haya yanatoka Gombelo, Wilaya ya Kilindi na kila siku napokea mahindi 1,000 mpaka 1,500 ambayo  tunagawana wafanyabiashara hapa na kuyachoma kisha kuwauzia wananchi," amesema.

Kwa siku nachoma mahindi zaidi ya mia moja na kuwauzia wananchi na imekuwa msaada mkubwa katika maisha yangu familia yangu inaponea hapa nasomesha na mahitaji mengine,” amesema Stephano.

"Hii pia ni baada ya mahindi mengi kunyauka hapa Kiteto kwa kutokuwa na mvua ya kutosha na kwa wakati  ambapo sasa tukaona changamoyo hii kuwa ni fursa kwetu kuuza mahindi mabichi," alisema Seif muuza mahindi mabichi Kibaya.

Hali hi imefanya uongozi wa wilaya ya Kiteto kuomba mahindi ya bei nafuu Serikalini ambapo hata hivyo hapa imeelezwa kuwa jitihaza za Serikali kusaidia wananchi hao chakula zimefanyika

"Hapa kata ya Kibaya kwa bahati mbaya tumepata changamoto ya gari kuharibika kwa sasa liko km tisa kufika hapa tunalenga tani 32 na bei imebadilika kutoka sh 800  kwa kilo hadi 700"  alisema...

Katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo aliyofanya hivi karibuni Kiteto na mkoa wa Manyara aliwataka wakulima na wanachi kutouza chakula chote kikiwa shambani

"Tunauza chakula chote tunaowauzia wanakuja kutulangua kwa bei mara tatu yake...sasa jifunzeni kuweka akiba ya chakula ukivuna acha kuuza mahindi yakiwa shambani acha kuuza siku umevuna unauza gunia elfu 40,000 unakuja kununua sh laki 120,000 akili hapo ipo? Alihoji Chongolo.