Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wahamasisha utoaji misaada sekta ya afya

Muktasari:

  • Banki ya NMB imetoa msaada wenye thamani ya Sh15 milioni kwa Hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda mkoani Mtwara, ikihamasisha utoaji wa misaada kwa sekta ya afya.

Mtwara. Wakati hospitali ya Rufaa ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi mkoani hapa ikitimiza miaka 96 ya utoaji wa huduma, wito umetolewa kwa wananchi kusaidia utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.

Hayo yameelezwa leo Februari 2, 2023 na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango alipokuwa akitoa msaada katika hospitali hiyo wenye thamani ya Sh15 milioni.

Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vitano vya kulazia wagonjwa wa kawaida pamoja na magodoro yake, mashuka 100, makabati madogo 10, vitanda vya wagonjwa wasiojiweza vitano, viti vya magurudumu vitano, stendi za kusimamishia dripu 10 na screen za hospitali tano.

 “Afya ni moja ya kipaumbele kwa Benki ya NMB na ni kutokana na ukweli kuwa afya ni msingi mkubwa sana kwa maendeleo ya Taifa lolote hapa duniani,” amesema Janeth.

Katibu wa Hospitali hiyo, Joseph Ndukusi Saiburu amesema kuwa msaada wa benki hiyo ni muhimu na umekuja wakati muafaka, ambapo hospitali hiyo inafanyiwa ukarabati mkubwa katika idara karibu zote.

“Tumefanya ukarabati wa wodi nyingi unaoenda kuweka vitanda vya kisasa na hivi vitanda ni gharama, msaada huu umekuja muda mzuri, tuna uhitaji wa vitanda 200 vya kisasa huu msaada umetuongezea nguvu, tuna mpango wa kununua kidogo kidogo kwa sababu ni ghali,” amesema Katibu wa hospitali.

“Hiyo pesa tutapeleka kwenye vitu vingine, tuna upungufu wa screen za hospitali (zile stendi ambazo zko pembeni ya vitanda) zinaongeza usiri kwa mgonjwa,” amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas ametoa rai kwa benki ya NMB kuendelea kufikiria vituo vingine vya afya na hata shule zilizo katika uhitaji.

Vile vile Kanali Abass ameiomba benki ya NMB kuendelea kubuni bidhaa na huduma nafuu zaidi ambazo mfanyakazi wa kawaida anaweza kumudu na kuzidi kuboresha huduma kwa wateja hasa watumishi wa afya.

“Nawapongeza sana NMB kwa kuchagua kutoa mchango wao wa vifaa tiba hapa hospitali ya Ndanda iliyopo wilayani Masasi mkoani hapa: amesema” Kanali Ahmed.