Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakazi Tarakea waomba kujengewa stendi

Muktasari:

Wananchi wanaouzunguka Mji wa Tarakea Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuwatengea eneo maalumu la stendi kutokana na eneo linalotumika kwa sasa kutokuwa na hadhi ya kuwa stendi.

  


Rombo. Wananchi wanaouzunguka Mji wa Tarakea Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuwatengea eneo maalumu la stendi kutokana na eneo linalotumika kwa sasa kutokuwa na hadhi ya kuwa stendi.

Mji huo wa Tarakea ambao upo mpakani mwa Kenya na Tanzania hauna stendi na badala yake Mabasi yaendayo mikoani pamoja na daladala zinalazimika kuegesha magari pembezoni mwa barabara hali ambayo inahatarisha usalama wa wananchi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Tarakea Motamburu, wananchi hao wamesema ipo haja ya Serikali kuangalia namna ya kuupanga mji huo na kutenga eneo la stendi kwa kuwa mji huo ndio kitovu cha biashara katika wilaya ya Rombo kutokana na mwingiliano mkubwa wa biashara uliopo katika eneo hilo.

Gody Mwaiyo, mkazi wa Tarakea amesema eneo hilo ambalo kwa sasa linalotumika kama stendi  imekuwa ni kero hata kwa wafanyaabishara kwa kuwa magari hayo yanaegeshwa pembezoni mwa biashara za watu.

"Watu wa Tarakea tunataka halmashauri itutafutie eneo ambalo litatumika kwa ajili ya matumizi ya stendi kwasababu hakuna stendi kabisa kwenye hili eneo, linalotumika ni  eneo la barabara ambapo pia ni mbele ya biashara za watu  jambo ambalo sio sahihi,"

Philibert Lyamuya, Mkazi wa Motamburu amesema eneo ambalo linatumika kama stendi imekuwa ni kero kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara wa eneo hilo kwa kuwa eneo hilo ni dogo na wakati mwingine linaweza kusababisha ajali.

"Hapa tulipo hatuna stendi ipo pembezoni mwa nyumba za watu na wakati mwingine watu wanashindwa kufanya biashara zao na kusababisha ajali tunaomba serikali  itufikirie kwa hili, maana hata eneo la wazi hatuna, anakuja kiongozi mkuu wa nchi hapa anazungumza na wananchi barabarani kutokana na kwamba hakuna maeneo,"amesema

Naye, Kimela Hashimu ambaye ni dereva wa Noah, zinazofanya safari Moshi-Rombo amesema kutokana na kukosekana stendi katika eneo hilo la Tarakea upakiaji wa abiria unakuwa ni mgumu kwa sababu  wanaegesha magari pembezoni mwa barabara.

Ofisa mipango miji wa Tarakea, Mwarabu Denis amesema ni kweli eneo hilo halina hadhi ya kuwa stendi na kwamba taratibu za upimaji ardhi zitakapokamiilika katika mji huo kutakuwa na utaratibu mzuri wa maeneo.