Wakulima wa ufuta washauriwa kuacha kilimo cha kuhamahama

Muktasari:

  • Wakulima wa zao la ufuta nchini wameshauriwa kuacha kilimo cha kuhamahama kwa dhana ya kukosa mavuno mengi badala yake watumie mbolea ya maji iliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari).



Mtwara. Wakulima wa zao la ufuta nchini wameshauriwa kuacha kilimo cha kuhamahama kwa dhana ya kukosa mavuno mengi badala yake watumie mbolea ya maji iliyofanyiwa utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari).

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa zao hilo, Joseph Nzunda wakati wa mafunzo yaliyofanyika leo Jumapili Aprili 24, 2022 kwa watafiti wa kituo cha Naliendele.

Amesema bado kuna tafiti zinaendelea kufanyika ili kumuwezesha mkulima kulima katika shamba moja na siyo kuhamahama.

"Ni kweli ufuta unakula chakula kingi kwenye ardhi lakini tumepata tiba ndio maana tunawashauriwa wasihame bali watumie watalaamu zaidi ili kuboresha mashamba yao ya ufuta kwa kufanya matumizi sahihi wakati majaribio mengine yenye tija zaidi yakiendelea kufanyika" amesema Nzunda

Kwa upande wake Mtafiti mstaafu wa zao hilo, Dk Omary Mponda amesema kuwa tafiti zinazoendelea nchini zina manufaa kwa wakulima na zinaleta tija katika zao hilo.