Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanafunzi 373 Karatu wanufaika na mradi wa vyoo wa Sh102 milioni

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha, Dk.Lameck Karanga akikata utepe kuzindua mradi wa Vyoo Shule ya Msingi Kambi ya Faru mradi uliojengwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa thamani ya Sh102.4 milioni. Picha na Filbert Rweyemamu

Muktasari:

  • Wanafunzi 373 wa Shule ya Msingi Kambi ya Faru, Karatu, wamenufaika na mradi wa vyoo vya kisasa wenye thamani ya Sh102 milioni uliojengwa na World Vision Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ya Karatu, ukiwa na lengo la kuboresha usafi, afya na mazingira ya kujifunzia.

Arusha. Wanafunzi 373 wa Shule ya Msingi Kambi ya Faru, Kata ya Kansay wilayani Karatu, wamenufaika na mradi wa vyoo vya kisasa wenye thamani ya Sh102 milioni uliotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania, kupitia Endabash Area Programme kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.

Akizindua mradi huo leo Juni 9, 2026, Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dk Lameck Karanga, ameutaka uongozi wa shule na wananchi kuutunza ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Amelishukuru shirika hilo kwa mchango wake katika kuboresha huduma za kijamii wilayani humo, akibainisha kuwa limetenga zaidi ya Sh2 bilioni kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, maji na ustawi wa jamii.

Ofisa Miradi wa World Vision Karatu, Fidelis Joseph, amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuimarisha afya na usafi shuleni.

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mkoa wa Arusha, Dk.Lameck Karanga akikata utepe kuzindua mradi wa Vyoo Shule ya Msingi Kambi ya Faru mradi uliojengwa na Shirika la World Vision Tanzania kwa thamani ya Sh102.4 milioni. Picha na Filbert Rweyemamu

Ameeleza kuwa mradi huo umehusisha ujenzi wa choo cha wavulana chenye matundu manne, choo cha wasichana chenye matundu matano, chumba maalumu cha usimamizi wa hedhi salama pamoja na kituo cha kunawia mikono chenye mabomba 10.

Joseph amesema mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa wa usafi binafsi, kupunguza magonjwa yatokanayo na uchafuzi wa mazingira na kuimarisha mahudhurio ya wanafunzi, hususan wasichana.

Mwalimu wa shule hiyo, Warda Said, amesema vyoo vipya vimeboresha mazingira ya shule na vitasaidia kuongeza mahudhurio ya wanafunzi wa kike kutokana na kuwepo kwa chumba maalumu cha usimamizi wa hedhi salama.

Amebainisha kuwa vyoo vya zamani vilikuwa vichakavu na vilikosa huduma ya maji, tofauti na miundombinu mipya ambayo imezingatia mahitaji ya sasa ya usafi na afya.