Wananchi walipwa Sh5 bilioni kupisha mradi wa gesi Lindi

Sunday March 07 2021
fidia pic
By Mwanja Ibadi

Lindi. Wananchi 674  wa vijiji vya Masasi, Likongo na Mtimkavu manispaa ya Lindi  wamelipwa fidia Sh5.2 bilioni ili waondoke katika maeneo yao kupisha mradi wa gesi wa LNG.


Kaimu  mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kelvin Kombo amesema  malipo ya awamu ya pili kupisha mradi wa gesi yamekamilika.


Akizungumzia malipo hayo mkuu wa Wilaya Lindi, Shaibu Ndemanga amewataka wananchi kutumiwa fedha hizo kwa ajili ya maendeleo yao na kuhakikisha wanaondoka katika maeneo yao ndani ya siku 90.


Advertisement

Malipo hayo yamefanyika baada ya yale ya Mei mwaka 2020 kukwama.


Imeandikwa na Mwanja Ibadi

Advertisement