Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake Chadema wafurika kumpokea Rais Samia


Moshi. Mamia ya wanawake wa  Chama Cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoka bara na visiwani tayari wamefurika katika viunga vya Ukumbi wa Kuringe mjini Moshi, wakimsubiri Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi kwenye Kongamano la Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Bawacha wafurika barabarani maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani

Wanawake hao waliingia kwa maandamano ya amani wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali ikiwemo yale ya Katiba Mpya.

Maandamano hayo yamefanyika leo asubuhi Machi 8, 2023 kutoka Soko la Kati hadi viwanja vya Ukumbi wa Kuringe yanakofanyika maadhimisho ya wanawake Bawacha kitaifa.
Rais Samia baada ya kumaliza kongamano hilo ataelekea Ofisi za CCM Mkoa wa Kilimanjaro saa saba mchana  na kusalimia wana CCM nje ya ofisi hizo.

Mpaka sasa viongozi mbalimbali wa Chadema wamewasili wakiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, John Heche, Peter Msigwa, Katibu Mkuu Bawacha, Catherine Ruge, John Mrema pamoja na viongozi wengine wa Kanda na mikoa.