Wapangaji wasio na mikataba waitwa NHC

Monday November 29 2021
nhc pic

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula

By Zourha Malisa

Morogoro. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula ametoa agizo kwa wapangaji wa  nyumba za biashara na makazi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wasiokuwa na mikataba na shirika hilo, wajitokeze ili wapate mikataba.
Akizungumza leo Jumatatu Novemba 29, 2021 katika kikao cha wahariri mkoani Morogoro, amesema wapo baadhi ya wapangaji waliopangisha  wapangaji walioingia mkataba na shirika hilo, jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu na  sheria za Shirika hilo.
"Wale wote ambao wanaishi kwenye nyumba za Shirika la nyumba na hawana mkataba nalo lakini ana mkataba na mpangaji, naomba ajitokeze na yeye ndiye atapata mkataba na shirika" amesema.

Advertisement