Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watano wafariki ajalini Kilimanjaro, wanne wajeruhiwa

Moshi. Watu watano wamefariki dunia papo hapo baada ya lori lililobeba katoni za maji ya kunywa kufeli mfumo wa breki katika eneo la mteremko barabara ya Mwika-Himo na kuigonga kwa nyuma gari dogo la abiria aina ya Toyota Noah lililokuwa likitokea Rombo kwenda Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Ajali hiyo imetokea jioni ya leo Jumapili Januari 15, 2023.

Daktari wa hospitali ya Faraja, Samweli Minja amethibitisha kupokea miili ya watu watano na majeruhi wanne.

"Ni kweli tumepokea miili ya watu watano wako mochwari na majeruhi wanne leo hapa hospitalini kwetu," amesema Dk Samweli

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza anaeleka eneo la tukio na atatoa taarifa baada ya kufika na kuona hali ilivyo

"Naelekea eneo la tukio kulikotokea ajali nikifika nitatoa taarifa kamili,"amesema Kamanda Maigwa


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi.