Watu 20 wafariki, 15 wajeruhiwa ajalini Kahama

Muktasari:

  • Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo trekta iliyotokea eneo la Mwakata Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.


Kahama. Watu 20 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu ikiwamo trekta iliyotokea eneo la Mwakata Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Ajali hiyo imetokea Saa 8:00 usiku wa kuamkia leo Jumanne, Agosti 9, 2022 ikihusisha gari ndogo aina ya IST, Hiace na Lori.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Kahama, Dk Deogratius Nyaga amethibitisha kupokea miili ya watu 20 na majeruhi 15 wanaoendelea kupatiwa matibabu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Shinyanga, Leonard Nyanduhu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema uchunguzi unaendelea.