Wawili wafungwa jela maisha kwa kubaka, kulawiti watoto

Muktasari:

  • Mahakama ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka mitatu na kulawiti mwingine wa miaka tisa.


  

Same. Mahakama ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa miaka mitatu na kulawiti mwingine wa miaka tisa.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mussa Hamza amesema mahakama imeridhika na ushahidi wa Jamhuri kuwa mkazi wa Mbuyuni katika Kata ya Gonja Maore, Jamal Hamis Abdallah (47) na Rashid Hamisi Bakari (52) maarufu kwa jina la Kifo, Kaya ya Makanya walitenda kosa hilo.

Jamal alifikishwa mahakamani Februari 8 mwaka huu na kushitakiwa kwa kumbaka mtoto wa miaka mitatu.

Kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha cha 130 (1) 2 (e) na cha 131 (1) vya Kanuni ya Adhabu.

Waendesha mashtaka wa Serikali, Frank Charles Masese na Samweli Flavian walidai mshtakiwa alitenda tukio hilo usiku wa Januari 29 mwaka huu katika Kata ya Gonja Maore.

Naye Rashidi Hamisi Bakari (52) mkazi wa Kitongoji cha Suji Kitivo alidaiwa kumlawiti kijana wa kiume wa miaka 9 aishiye katika kitongoji hicho. Alidaiwa kutenda tukio hilo tarehe 18/0/2021 majira ya mchana.

Hakimu Hamza alisema alisema ushahidi uliotolewa na waathirika na mashahidi wengine wa Jamhuri haukuacha shaka kuwa washtakiwa walifanya unyama huo na kuwapa adhabu ya kifongo cha maisha kila mmoja.

Imeandikwa na Dickson Mnzava, Mwananchi