Waziri Mkuu India aeleza umuhimu reli ya Kashmir

Waziri Mkuu India aeleza umuhimu reli ya Kashmir

Muktasari:

Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameagiza ujenzi wa reli inayounganisha majimbo ya Jamuu na Kashmir nchini humo kukamilika kabla ya Agosti 15, 2022.

Modi aliyasema hayo wakati wa mkutano wake kwa njia ya video na makatibu wakuu wa nchi hiyo na kuhoji maendeleo ya mradi huo.

New Dehli, India. Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi ameagiza ujenzi wa reli inayounganisha majimbo ya Jamuu na Kashmir nchini humo kukamilika kabla ya Agosti 15, 2022.

Modi aliyasema hayo wakati wa mkutano wake kwa njia ya video na makatibu wakuu wa nchi hiyo na kuhoji maendeleo ya mradi huo.

Alisema mradi huo ni muhimu si tu katika kurahisisha usafiri kwa wananchi katika majimbo hayo bali pia kudumisha usalama katika eneo hilo ambalo kwa muda mrefu limetawaliwa na mapigano.

Alisema mradi huo utasaidia kupunguza umasikini kwa wananchi hao ambao wamekuwa wakikamiliwa na umasikini uliokithiri pamoja na magonjwa mbalimbali.

Ili kukuza utalii na uchumi katika eneo hilo, Waziri Mkuu aliagiza mradi wa reli kukamilika ifikapo Agosti 15, 2022 ili wananchi waanze kunufaika.

Serikali ya India pia inatekeleza mipango mingine katika jimbo la Jammu na Kashmir ikiwa ni pamoja na huduma za afya kwa gharama nafuu pamoja na maji safi na ya kutosha ifikapo mwaka 2024.

Jitihada hizo zitasababisha uboreshaji wa hali za maisha ya jamii za vijijini na kwa hivyo lazima ichukuliwe katika maeneo yote. Iliarifiwa kuwa huko Jammu na Kashmir, malengo umekamilika katika wilaya mbili na zingine zitakamilika ifikapo 2022.

Jammu na Kashmir ni eneo linalimilikiwa na India kama muungano, ambalo upande wa kusini ni sehemu ya Kashimir ambayo imekuwa katika mgogoro kati ya Indi a na Pakistan tangu mwaka 1947, na kati ya India na China kwa upande mwingine tangu mwaka 1962.