WhatsApp kuzuia watumiaji kutuma, kupata ujumbe

WhatsApp kuzuia watumiaji kutuma, kupata ujumbe

Muktasari:

  • Watumiaji wa mtandao wa WhatsApp, ambao hawakubaliana vigezo na masharti mapya, hawatapokea wala kutuma ujumbe wowote kuanzia Mei 15, hadi

Dar es Salaam. Watumiaji wa mtandao wa WhatsApp, ambao hawakubaliana vigezo na masharti mapya, hawatapokea wala kutuma ujumbe wowote kuanzia Mei 15, hadi watakapokubaliana nayo.
Akaunti zao zitaonekana kama "haziko hai" na akaunti ambazo haziko hai zinaweza kufutwa baada ya siku 120.
Miito na taarifa zitaendelea kufanya kazi "kwa muda" lakini, TechCrunch imeripoti, inawezekana kwa "wiki chache".
WhatsApp ilitangaza kuhuisha (update) mtandao huo kuanzia Januari.
Kuna hisia tofauti kwa watumiaji wengi wanaodhani kuwa mpango huo unamaanisha kuwa kampuni hiyo inapanga kubadili kiwango cha taarifa inachochangia na kampuni mama ya Facebook.
Kampui hiyo ilifafanua baadaye kuwa hakuna mpango huo - bali unamaanisha kuwezesha malipo kufanyika katika  biashara.
Tayari WhatsApp inapena baadhi ya taarifa na Facebook, kama vile anuani ya IP ya mtumiaji (mlolongo wa namba zilizoambatanishwa katika kila simu na kuunganishwa na internet, zinaweza pia kutumiwa kuonyesha ilipo) na malipo kufanywa kwa kutumia mtandao huo.
Lakini hilo halifanyiki barani Ulaya na Uingereza, ambako kuna sheria tofauti za faragha.
Baada ya taarifa ya awali, mitandao kama Telegram na Signal ilipata ongezeko la watumiaji wakati wateja wa WhatsApp wakitafuta mbadala wa huduma ya kutumiana ujumbe.
WhatsApp ilichelewesha utekelezaji wa awali na sasa imebadilisha njia ya kuwataarifu watumiaji kuhusu mabadiliko hayo.