Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wizara yawanoa waandishi Lindi huduma mtandao kwa wananchi

Baadhi ya waandishi wa habari Mkoa wa Lindi wakiwa kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria, yaliyofanyika katika ukumbi wa Seaview mkoani Lindi.

Muktasari:

  • Mfumo huo unalenga kupunguza gharama na umbali kwa wananchi wanaotafuta haki. Wizara ya Katiba na Sheria yasema waandishi ni daraja la kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya mfumo huo.

Lindi. Zaidi ya waandishi wa habari 30 wa Mkoa wa Lindi wamepata mafunzo ya siku moja yaliyoandaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria ya kuwajengea uwezo wa matumizi ya mfumo wa kutoa malalamiko au taarifa katika kituo cha huduma mtandao.

Malengo ya kuanzisha kituo hicho ni kupunguza gharama kwa wananchi waliokuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za kisheria.

Akifungua mafunzo hayo leo Juni 9, 2026, Wakili wa Serikali kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Erick Salila, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili wawe mabalozi wa kuwafikishia wananchi elimu kuhusu njia sahihi ya kupata haki na kutoa taarifa za ukiukwaji wa sheria kupitia huduma ya mtandao.

Amesema hadi sasa kituo hicho cha Katiba na Sheria kimeshapokea malalamiko zaidi ya 2,000, na baadhi ya malalamiko yameshafanyiwa kazi na mengine yapo kwenye utekelezaji.

“Hii huduma inasaidia kupunguza gharama kwa mwananchi kwenda kutafuta haki katika vyombo vyetu vya sheria. Sasa hivi hata ukiwa kijijini, unawasiliana na kituo chetu, unatoa malalamiko yako, tunayafuatilia na kuyafanyia kazi,” amesema Wakili Salila.

Aidha, Wakili Salila amefafanua kuwa waandishi wa habari ni daraja kati ya Serikali na wananchi, hivyo amewataka kwenda kuwaelekeza wananchi jinsi ya kutumia kituo cha huduma mtandao kuripoti changamoto zinazohusiana na haki, sheria na utoaji wa huduma, kwani itapunguza foleni na kuongeza uwazi.

Ameongeza kuwa kituo hicho cha mtandao kimeundwa ili mwananchi aweze kutoa taarifa yake kwa urahisi bila hitaji la kusafiri umbali mrefu kwenda ofisini.

Mwandishi wa habari kutoka ZBC, Hadija Omary, amesema kuwa mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka, kwani mara nyingi wananchi hukosa mwelekeo wa kutoa malalamiko yao.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukipata taarifa kutoka kwa wananchi lakini hatujui njia sahihi ya kuwashauri. Sasa tumejifunza jinsi ya kuwasaidia waingie kwenye mfumo na kuwasilisha taarifa zao wenyewe,” amesema Omary.