Yanga SC, Namungo FC mbele kwa mbele VPL

Yanga SC, Namungo FC mbele kwa mbele VPL

Muktasari:

Yanga SC inaikaribisha Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaoanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo, huku kocha wa kikosi hicho Cedrick Kaze akifurahia baada ya wachezaji wake Mukoko Tonombe na Lamine Moro waliokuwa majeruhi kuwa fiti kwa mchezo huo.

Dar es Salaam. Yanga SC inaikaribisha Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaoanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo, huku kocha wa kikosi majeruhi kuwa fiti kwa mchezo huo.

Lamine hicho Cedrick Kaze akifurahia baada ya wachezaji wake Mukoko Tonombe na Lamine Moro waliokuwa aliumia katika mchezo dhidi ya Simba uliofanyika Novemba 7 na kutolewa dakika ya 48 wakati Mukoko aliumia mazoezini, hivyo wote walileta wasiwasi wa kutocheza mchezo wa leo lakini habari kutoka ndani ya kambi ya timu hiyo zinasema wote wamepona na kocha anaweza kuwatumia.

Namungo ambayo hivi karibuni imemtimua kocha wake Hitimana Thierry na kumchukua Hemed Morocco, imepania kuharibu rekodi ya Yanga ya kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mchezo kwenye Ligi Kuu.

Kocha Morocco alisema anaiheshimu Yanga na amekuwa akiifutilia, lakini haihofii kwani mpira ni uwanjani hivyo dakika 90 za mchezo ndizo zitaamua.

“Najua ndio kwanza mgeni ndani ya Namungo, lakini wachezaji ni walewale hivyo mechi yangu ya kwanza ni dhidi ya Yanga. Nawaheshimu wapinzani wetu kwani kwa sasa wako vizuri sababu hawajapoteza mchezo hata mmoja, lakini hilo halitufanyi kuwahofia kwani mpira ni uwanjani, hivyo watu wasubiri kuona,” alisema Morocco.

Yanga na Namungo zimekuwa na upinzani mkubwa kila zinapokutana kwani msimu uliopita timu hizo zilitoka sare katika mechi zote mbili za ligi- zikitoka sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofanyika Machi 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa na mabao 2-2 katika mchezo uliofanyika Juni 24 jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wa kocha wa Yanga, Kaze alisema hakuna mchezo rahisi kwao na kwamba, mabadiliko ya Namungo katika kuleta kocha mpya yataongeza ugumu wa mchezo huo kwa kuwa kila mchezaji atataka kuonyesha kitu kwa kocha mpya.

Kaze alisema hesabu zao ni kutafuta pointi tatu na tayari maandalizi yako vizuri ambapo wamepata muda wa kuzifanyia kazi changamoto zao katika kutumia nafasi za kufunga.

“Tumesikia wamebadili kocha, hii ni changamoto nyingine ya ugumu wa mchezo itafanya kila mchezaji wao kujituma, nafahamu ni timu nzuri (Namungo) wanakaribia kuanza mashindano ya Shirikisho barani Afrika, ina maana mchezo huu ni sehemu ya kujipanga kwao,” alisema Kaze.

“Tumejipanga vyema kwa mchezo huu, tulikuwa na wachezaji wachache waliokuwa na maumivu kidogo ingawa sio sana na sasa naona kila kitu kipo sawa, tunahitaji kutumia nafasi tunazotengeneza vyema uwanjani, tumeyafanyia kazi hayo tusubiri kuona mrejesho kutoka kwa vijana.”

Mbali ya Yanga na Namungo kuumana mchezo mwingine wa leo utakuwa kati ya Kagera Sugar itakayoikaribisha Mwadui FC kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.