Zitto: Rais Samia kaanza vizuri lakini tusibweteke

Zitto: Rais Samia kaanza vizuri lakini tusibweteke

Muktasari:

  • Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoapishwa kushika madaraka baada ya kifo cha hayati John Magufuli, wananchi wamekuwa na matumaini makubwa na utawala wake, lakini ameonya hawapaswi kubweteka na utawala huo.

Dar es Salaam. Kiongozi wa Chama cha ACT - Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema tangu Rais Samia Suluhu Hassan alipoapishwa kushika madaraka baada ya kifo cha hayati John Magufuli, wananchi wamekuwa na matumaini makubwa na utawala wake, lakini ameonya hawapaswi kubweteka na utawala huo.

Rais Samia aliapishwa Machi 19 baada ya kifo cha Rais Magufuli, aliyefariki Machi 17 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisi za Mwananchi zilizoko Tabata Relini jijini Dar es Salaam, Zitto alisema Rais Samia ana jukumu kubwa la kulinda imani anayopewa na wananchi kwa kufanya mabadiliko ya kisheria ya mifumo iliyopo sasa.

“Nyinyi pia ni mashahidi, tangu tumempata Rais Samia kumekuwa na matumaini makubwa ya wananchi. Mimi nimetoka nje ya Dar es Salaam, juzi nilikuwa Mwanza, jana nilikuwa Kibondo (Kigoma), unaona kuna mabadiliko makubwa. Matumaini ni makubwa.

“Naamini kabisa Mama Samia hatawaangusha Watanzania. Bali mabadiliko haya haya yatakuwa ya kiuchumi na mabadiliko ya kutenda haki. Kama mlivyosikia amesema hataki dhulma, ina maana katika maisha yake yote anasema hataki dhulma,” alisema Zitto.

Huku akitoa mfano wa wafanyabiashara wa fedha za kigeni jijini Arusha waliotakiwa kusalimisha fedha zao Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Zitto alisema Rais Samia amewatoa Watanzania kwenye enzi za kudhulumiwa na kunyimwa uhuru wa maoni.

Soma zaidi gazeti la mwananchi leo