Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hekaya za Mlevi: Kicheko kikizidi hugeuka kilio

Muktasari:

  • Tuliamini kuwa alikuwa akitengenezea kicheko cha kupunguza msongo, lakini hatukuwa na uhakika. Wakati mwingine alituudhi kwani wakati tunashauriana namna ya kuyakwepa majanga yetu, yeye anacheka.

Dar es Salaam, Kuna kijana mwenzetu alipata shida sana wakati ule tukiwa shuleni. Yeye hakuwahi kukasirika wala kugombana na mtu, bali alitumia muda mrefu kusikiliza stori na kucheka hata kama stori hizo hazikuchekesha.

Tuliamini kuwa alikuwa akitengenezea kicheko cha kupunguza msongo, lakini hatukuwa na uhakika. Wakati mwingine alituudhi kwani wakati tunashauriana namna ya kuyakwepa majanga yetu, yeye anacheka.

Shida ilikuja pale tulipokosea na kuadhibiwa kwa viboko na walimu. Wakati sisi wenzake tukipiga kelele za maumivu na kusaga meno, yeye alipaza sauti bila machozi. 
Lakini mara tu alipoachiwa aliangua kicheko! Aliwaudhi walimu na akatuudhi zaidi tulipokwenda bwenini kuugulia moto wa bakora. Yeye alirejea kwa vitendo jinsi tulivyokuwa tukigaragara huku akicheka. 

Ilifikia mahala alipelekwa kwenye Hospitali ya Rufaa kuchunguzwa iwapo ana tatizo la ubongo.  

Kicheko ni kirutubisho cha afya ya mwili na akili. Ilinenwa “kama huna makunyanzi basi hujacheka vya kutosha”. Walimaanisha ili uufikie uzee, acha mambo ya bifu, visirani na kununanuna. 

Watu wa Pwani husema kwa kejeli, “We ukisusa sie wenzio twala!” Ni kama usemi wa watoto wakiwa wanagombania chakula chako, ukiona kero na kususa wenzio watakula huku wakikukejeli kwa kukuonesha hadi magego yao yanavyogegeda mifupa. Hapo ni lazima utalia.

Lakini kila dawa inapaswa kutumika kwa uangalifu. Vijana wa miongo iliyopita watakubaliana nami kuwa katika wakati wetu tulikuwa waangalifu sana kwenye mahusiano. 
Ukimpiga kibuti mpenzi wako atakimbilia kumeza vidonge vya klorokwini ili afe na kukuacha ufaidi na hao wanaokuzuzua. Tulishuhudia wasichana wengi wakipoteza maisha kwa dawa hiyo iliyokuwa kuu kwa ugonjwa wa malaria.

Hivyo kicheko kinapaswa kutumika kwa furaha yako na watu wengine. Kikitumika vinginevyo kinaleta uadui na hasara. Hii inanikumbusha mama mmoja aliyekuwa akimfuga kasuku aliyempenda sana. 

Wengi wanadhani kasuku anajua kuongea, lakini kumbe anachojua ni kuiga maneno. Ukitaka kuamini kaa naye uanzishe stori. Hatakujibu zaidi ya kurudia yaleyale unayoyasema. 

Basi ikawa siku moja yule mama alikuja kudaiwa hela za marejesho. Siku hiyo hakuwa na kitu, hivyo akamsihi kijumbe ampe muda zaidi.

Kama unavyowajua vijumbe wa uswahilini, mama alichambwa na mchambaji aliondoka na maneno ya kejeli yaliyoishia na kicheko kikali halafu kirefu. Siku hiyo iliharibika asubuhi na mapema, mama akabaki analia kila alipokumbuka kejeli na kicheko kile.

Kwa bahati mbaya kasuku akashika maneno pamoja na kile kicheko. Akawa akiyarudia kila alipomwona yule mama, jambo lililomtesa mama yetu. Asubuhi moja mama aliamka na taarifa za mwanaye kusitishwa masomo kwa ukosefu wa ada. Wakati anajiandaa kwenda kupiga misele akakutana na kicheko cha kasuku: “He-heeeee! Utalipa...”

Mama hakufikiria mara mbili; alimtia kasuku kwenye kiroba na kuondoka naye. Hatujui alikwenda kumuuza au kumtupa. 

Kicheko kina faida na hasara. Ndege wanaokula nyama husafiri na wawindaji kama simba na chui, wakipata mawindo basi nao wanaambulia. Lakini fisi japokuwa wanakula mifupa, wamejenga uadui mkubwa na chui asiyeihitaji mifupa hiyo.

Baada ya chui kushiba hujipumzisha mtini, fisi watavamia mifupa huku wakicheka. Chui hudhani anachekwa yeye kwa majeraha aliyoyapata mawindoni, hivyo hushuka na kuwatimua fisi. Hii ndiyo hasara ya kicheko cha hovyo.

Mtaani kwetu watu wana maudhi sana. Mnaelekea kupishana, unamwona tangu akiwa mbali anakuja akiwa mtulivu. Lakini wakati mnapishana anakutupia jicho na kutikisa kichwa kwa namna ya kusikitika, kisha anaangua kicheko cha tumboni akijizuia kufungua mdomo. 
Unamuuliza kuna nini, yeye anacheka laivu na kutokomea. Ingelikuwa wewe ndiye uliyekutana naye ungefanyaje kama si kurudi nyumbani na kujiangalia upya.
Lakini ukute huyo mtu aliamua kukushughulisha tu bila sababu. 

Wapo watu wengi wanaokosa mambo ya kufanya, mbaya zaidi hawataki kujifunza kutoka kwa wengine. Na wapo ambao wameumbwa na uchokozi, wale ambao wakiona mbwa amefungwa getini wanapatwa na hamu ya kumrushia mawe. Hawa wanachohitaji kuona ni hasira za mbwa ni za kiasi gani.

Nakumbuka utotoni tulikuwa na michezo ya kuchimba shimo la urefu wa mkono, tukalifunika vizuri kwa nyasi na udongo kulificha. Mwenzetu aliyekanyaga hapo na kutumbukia ndiye aliyekuwa burudani yetu, lakini mara zote michezo kama hiyo huisha kwa vilio baada mtego kumnasa mtu asiyekusudiwa anaweza kuwa baba au jirani aliyekuja nyumbani kusalimia. Tulikula mikwaju hadi tukausahau mchezo wenyewe. 

Naiona hiyo hata kwa viongozi wetu huku mtaani. Wanaangalia mzuka wa wananchi wanaowaongoza na kuwafanyia jambo lolote baya litakalogusa hisia zao. Wenyewe wanaamini kuwa ndio walioshika mpini wa kisu, hivyo watakaoshindana nao wataishia kujikata vidole. Ukitafakari utaona hawakuwa na sababu ya kufanya hivyo, ila kutafuta kicheko baada ya washindani wao kuumia. 

Siku moja kulizuka mzozo wakati wa urudishwaji wa fomu za kura za maoni katika moja ya mitaa ya uswahilini. Wakati vumbi la wadai haki likielekea kuwachafua, viongozi walifunga ofisi na kualikana sehemu. Waliketi wasipoonekana wakiwacheka. Kwa lugha ya katuni, nilimwona mtu niliyekuwa namdai shilingi elfu tano akilipia taksi ya shilingi elfu kumi na kunikimbia huku akinicheka ninavyohangaika. Hakyanani nikimkamata...