Kichochezi hiki kwa wanaume, muhimu kutungisha mimba

Friday January 01 2021
wanaume pic

Kichochezi cha Testosterone ndiyo nyenzo muhimu kwa mwanaume kuweza kutungisha mimba, kuwa na misuli mikakamavu, mtawanyiko wa mafuta mwilini na utengenezwaji wa chembe hai nyekundu.

Inapotokea kiwango cha kichochezi hiki kuwa chini kuliko kawaida mwanaume hupata matatizo kama vile kusinyaa kwa maumbile ya kiume na ugumba.

Kutokana na kuendelea kwa maendeleo ya kisayansi upande wa uchunguzi miaka ya sasa imewezesha kugundulika upungufu wa kichochezi hiki kwa baadhi ya wanaume.

Tatizo hili limechangia uwapo wa uhitaji virutubisho maalumu vya kuchochea utengenezwaji wa kichochezi hiki mwilini mara tano zaidi kuliko miaka kumi iliyopita.

Kwa kawaida kokwa za kiume hutengeneza vichochezi vya kiume vinavyojulikana kama Androgens, kazi zake ni kuchochea ukuaji wa mfumo wa viungo vya uzazi, misuli imara, sauti nzito na sauti ya bezi vile vile kupata ashiki ya kujamiiana.

Kichochezi cha Testosterone ni moja ya aina muhimu ya Androgen inayojulikana zaidi. Kwa kawaida kokwa zenye afya huweza kutengeneza mbegu miligramu 6 kwa siku.

Advertisement

Vile vile kwa kokwa za kiume hutengeneza karibu wastani wa mbegu za kiume 200,000 kwa dakika, ingawa mwanaume (miaka 30 zaidi) kiwango chake hupungua.

Ukiacha athari inayosababishwa na umri yapo matatizo ya kiafya yanayosababishwa au kuchangia kupungua kwa kiwango cha Testosterone, kwa kawaida mwanamume aliyezaliwa bila hitilafu ya kimaumbile huwa na kokwa mbili (testicle) au hujulikana pia kama kende, huundwa ndani ya tumbo kabla ya kuzaliwa na hapo baadaye hushuka wakati mimba ikiwa na miezi saba.

Katika hatua hii baadhi ya watoto huweza kuzaliwa na hitilafu ya kende kutoshuka na katika pochi yakuhifadhia kokwa. Tatizo hili huwapata asilimia mbili ya watoto wakiume wanaozaliwa huku asilimia 10 ya wanaozaliwa kokwa zote mbili zikiwa zimakaa vibaya. Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu

_______________________________________________________________

Makala hii imeandikwa na Dk Shita Samwel

Advertisement