TEKNOLOJIA: Jinsi ya kuchaji simu janja ijae kwa haraka zaidi

Teknolojia inarahisisha mambo mengi ikiwamo kuokoa muda. Miongoni mwa teknolojia rahisi ni matumizi ya simu janja, ambazo baadhi yake zinakwisha chaji haraka. Lakini zipo mbinu za kukusaidia kuijaza haraka pia katika simu yako janja.

Kwanza ukiiweka katika chaji ili ijae haraka weka airplane mode. Itakusaidia kwa sababu chaji inayoingia au iliyopo katika simu haitatumika., hivyo inayoingia itakwenda moja kwa moja katika betri.

Pia zingatia siku zote usitumie chaji iliyopo katika simu hadi imalizike kabisa. Ikiwa na chaji hata jino moja inakuwa rahisi kupokea moto haraka na kujaa.

Pia simu ikichajiwa katika joto inaweza isijae haraka na betri likapata moto, hivyo kwa matokeo mazuri ichajiwe eneo ambalo lina hewa ya kawaida.

Ndiyo maana pia ili kuiepusha simu na joto kali, unashauriwa pia kuichaji ikiwa haina kava. Hivyo kama simu ina kava ni vema kujenga utamaduni wa kulivua wakati wa kuchaji hadi ikijaa ndiyo livalishwe.

Simu ikichajiwa na chaja yake halisi itafanikisha kujaa haraka.