🔴#LIVE: Mkutano wa CCM siku ya pili waanza Dodoma

Mkutano wa CCM siku ya pili waanza Dodoma

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan ameshaingia katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuendelea na Mkutano Mkuu siku ya pili leo.

Dodoma. Mwenyekiti wa CCM Samia Suluhu Hassan ameshaingia katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kuendelea na Mkutano Mkuu wa chama hicho siku ya pili.

Rais Samia ameingia katika geti Kuu saa 3.00 asubuhi na moja kwa moja msafara wake ulielekea katika Ofisi za chama makao makuu zilizopo ndani ya majengo ya ukumbi huo.

Leo Alhamisi Desemba 8, 2022 mkutano utapokea na kujadili utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo itawasilishwa na Waziri Mkuu kwa Serikali ya Muungano na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar kwa upande wa pili wa Muungano.

Kwa mujibu wa ratiba, kutakuwa na ratiba ya Utekelezaji wa Kazi za chama ambayo itawasilishwa na Naibu Katibu Mkuu, majadiliano na maazimio ya mkutano mkuu.

Kabla ya kuahirishwa kwa mkutano Makamu Wenyeviti pande zote watatoa maneno ya shukrani kwa wajumbe.

Mkutano Mkuu utaahirishwa mchana na kisha jioni wajumbe wataendelea na Kikao Cha kwanza cha Halmashauri Kuu Kikao kinachotazamiwa kutoa mwelekeo wa sekretarieti ya CCM.

Kabla ya kuingia wajumbe ndani, nje ya ukumbi wajumbe wa NEC Dk Mwigulu Nchemba na Innocent Bashungwa walikuwa wakigombewa kupiga picha na wajumbe.