ACT wazalendo kuzindua mikutano ya hadhara Februari 19

Muktasari:

 Siku moja baada ya Chadema  kuzindua mikutano ya hadhara jijini Mwanza, Chama cha ACT wazalendo nacho kimetangaza kuanza mikutano yake Februari 19, 2023 jijini Dar es Salaam.Dar es Salaam. Siku moja baada ya Chadema  kuzindua mikutano ya hadhara jijini Mwanza, Chama cha ACT wazalendo nacho kimetangaza kuanza mikutano yake Februari 19, 2023 jijini Dar es Salaam.

Akisoma maamizio ya kamati kuu ya chama hicho iliyoketi jana Dar es Salaam, katibu mkuu wa ACT wazalendo,  Ado Shaibu amesema, "katika awamu ya kwanza programu ya kitaifa ya mikutano ya hadhara  inajumuisha mikoa ya Dar es Salaam Februari 19 Unguja, 26 Februari Pemba,  Machi 4 Tanga na Pwani ni Machi 9."

"Pia Lindi mkutano tutafanya Machi 10, Mtwara Machi 11, mkoa wa kichama Selous Machi 12, Tabora Machi  14-15 na Kigoma Machi 16-18."

Kuhusu awamu ya pili ya mikutano hiyo, Shaibu amesema itatangazwa baadaye akibainisha kuwa  ajenda zitakazotawala mikutano ya ACT Wazalendo ni hali ya maisha ya wananchi na mageuzi ya mifumo ya kidemokrasia nchini na kitambilisha ahadi za chama hicho.

"Chama kinatambua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi, namna watawala wameshindwa kuzitatua, sisi tutaonesha sera mbadala za  kutatua changamoto hizo,"amesema.

Amesema kabla ya kuzindua mikutano ya hadhara, Februari 18, 2023 watazindua kaulimbiu ya chama hicho.