Lukuvi, Simbachawene watoswa CCM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), George Simbachawene akifuatilia uchaguzi wa kugombea ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa katika uchaguzi uliofanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa chama hicho, jijini Dodoma leo.

Muktasari:

  • Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, wamewatosa vigogo wa chama hicho, akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), George Simbachawene pamoja na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi.

Dar es Salaam. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, wamewatosa vigogo wa chama hicho, akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), George Simbachawene pamoja na Mbunge wa Isimani, William Lukuvi.
Wengine waliotoswa katika uchaguzi wa chama hicho, uliofanyika leo Jumatano, Desemba 7, 2022 Jijini Dodoma ni pamoja na Katika matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Dk Ali Mohamed Shein kwenye ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma yameonesha vigogo hao na wengine  wakishindwa kupenya katika kundi la wagombea wanaume wa Tanzania bara ambapo nafasi 14 zilikuwa zikiwaniwa.
Pia, katika matokeo hayo yumo Naibu Waziri wa Ofisi Rais (Utumishi na Utawala Bora), Deo Ndejembi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Geofrey pinda, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Jumanne Sagini.
Wengine ni waziri wa zamani wa Kilimo, Japhet Hassunga na mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba Naibu Waziri, Yupo pia mbunge wa zamani wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir na mbunge wa Ukonga Jerry Silaa.