Makada, wabunge na mawaziri kuchuana U-NEC CCM

Dodoma. Ni vita ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge na mawaziri katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi kuwania nafasi tatu za ujumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC), Tanzania Bara.

Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi unafanyika leo Alhamisi Novemba 24, 2022 katika ukumbi wa Chuo cha Mipango jijini Dodoma.

Uchaguzi huo umefunguliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Abdulrahman Kinana ambapo wajumbe 832 wanatarajia kupiga kura katika uchaguzi huo.

Katika nafasi ya mwenyekiti wanaogombea n inane akiwemo mwenyekiti anayetetea nafasi hiyo, Dk Edmund Mndolwa. Pia wamo, Bakari Kalembo, Fadhil Mohammed Maganya.

Wengine ni Said Mohammed Mohammed (Dinya), Mwanamanga Juma Mwaduga, Ally Maulid Athumani, Ally Khamis Masoud na Zahara Hassan Haji.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wanaogombea ni Haidar Haji Abdallah, Dk Wemae Alen Chamshama, Fatma Abeid Haji, Rachel Ngiganyingwa Kabunda, Dk Neema George Mturo, Zahoro Salehe Mohammed na Dogo Iddi Mabrouk.

Mbali ya nafasi hizo, makada wa CCM ambao ni mawaziri na wabunge kama, Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.

Wengine ni Mbunge wa Viti Maalum, Bupe Mwakang'ata, Nyiriza Nyiriza, Mgore Kigera, Kelvin Tegwa, Paul Kirigini, Mecktridis Mdaku.

Pia kuna, George Gandye, Mohammed Ngingite, Daniel Sayi na Hamoud Abuu Juma.

Wajumbe wa mkutano huo, wamemchagua, Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa wa Kilimanjaro, Daudi Mrindoko kuwa mwenyekiti wa muda wa uchaguzi huo ambaye anasaidiana na Msimamizi Mkuu Maalum, Kombo Hassan.


Endelea kufuatilia mitandao yetu kwa habari zaidi.