Sabaya mwenyekiti mpya wa CCM Arusha

Muktasari:

  • Sabaya ameongoza kwa kura 463 katika uchaguzi mdogo wa nafasi hiyo uliofanyika leo Desemba 4, 2023 katika ukumbi wa mikutano ya AICC Mkoani Arusha.

Arusha. Thomas Ole Sabaya amefanikiwa kuibuka mshindi wa nafasi ya uenyekiti mkoa wa Arusha, baada ya kupata kura 463 na kuwabwaga wapinzani wake watatu.

Sabaya aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti ambaye pia ni baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefanikiwa kushinda kiti hicho katika uchaguzi mdogo wa nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Steven Zelothe.

Msimamizi wa uchaguzi wa CCM Anthony Mtaka, amesema leo Desemba 4, 2023, walitarajia wajumbe 1001 lakini waliopiga kura jumla walikuwa 906 na moja iliharibika.

Amesema kuwa wagombea wanne waliteuliwa na kupigiwa kura ambapo Sabaya ameshinda kwa kura 463.