Shaka awapa ujumbe wagombea uchaguzi CCM

Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Shaka Hamdu Shaka akipiga kira. Picha na Jesse Mikofu

Muktasari:

Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikifanya chaguzi za wenyeviti wa Mikoa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa na Taifa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho,  Shaka Hamdu Shaka, amesema viongozi hao ndio wanategemewa kukivusha chama katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Unguja. Wakati Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikifanya chaguzi za wenyeviti wa Mikoa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa na Taifa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho,  Shaka Hamdu Shaka, amesema viongozi hao ndio wanategemewa kukivusha chama katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.


 Amesema chaguzi hizo ni muhimu kwa chama hicho na kuwataka wajumbe kuchagua viongozi makini na wenye maono.


Ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 20, 2022 wakati wa uchaguzi huo katika Mkoa wa Magharibi ambapo amesema chaguzi hizo zinakiwezesha chama kupanga safu yake.


Amesema viongozi watakaochagulia katika chaguzi hizo watakuwa na dhamana kuhakikisha chama kinabaki salama kinaendelea kusimama imara katika kutete ibara ya nne ya chama hicho ya kwamba kila inapofika nyakati za uchaguzi lazima kishinde na kushika atamu za uongozi.


"CCM ndio kimbilio na tumaini la Watanzania, kwahiyo viongozi ambao wataokapatikana leo watambue wanadhamana ya kuwa kiunganishi baina ya chama na Serikali hasa katika kuisimamia Serikali ya Zanzibar na ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa ilani ya chama hicho," amesema


Amesema CCM iliwaahidi watanzania kwamba ndani ya kipindi cha miaka mitano 2025, kazi kubwa ambayo kitafanya ni kuwaletea Maendeleo endelevu, kiuchumi, kijamii na kisiasa na kwamba kazi hiyo inafanywa vyema katika Serikali zote mbili na mafanikio yaliyofikiwa yanaonekana kwa macho na jinsi taifa linavyozid kufunguka.


Amesema Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi amefanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Wazanzibar na kugusa Ustawi wa maisha yao, kubwa ni kuwakumbusha tu kwamba viongozi watakaopewa dhamana leo hii wanajukumu kubwa kupeperusha bendera ya chama kulinda maslahi ya chama chetu.'


Katika nafasi ya Mwenyekiti wa Mkoa, wagombea wapo watatu ambapo kila mmoja amepewa dakika tatu kuomba kura kwa wajumbe wa mkutano huo.


Hata hivyo, mgombea mmoja, Asha Makungu Othman hakuwapo kwenye mkutano huo.


Akiomba kura, Said Yassir, amewaomba wajumbe hao wamchague kwasababu anauzoefu wa muda mrefu ndani ya chama hicho.


"Nimekuwa Katibu wa vijana hapa Zanzibar kwa miaka tisa, lakini nimekuwa Katibu wa vijana Mikoa mbalimbali Tanzania Bara na mwisho nilikuwa Dar es Salaam sasa nimeletwa tena nyumbani, naomba kura zenu," amesema Yassir


Naye Mohamed Rajab Soud anayetetea nafasi hiyo, amesema amekuwa nao kwa kipindi cha miaka mitano hivyo wanajua mengi aliyoyafanya bila kuyaeleza.


"Nilikuwa nanyinyi kwa kipindi cha miaka mitano, sina la kusema imani yangu tutakuwa pamoja kwa kipindi kingine," amesema


Msimamizi wa uchaguzi huo, Mattar Zahor Masoud amesema wajumbe wapo 408, lakini waliohudhuria ni 400,