Rais Samia sikia kilio chetu sisi Twea, tunaomba huruma yako

Muktasari:

  • Chama cha wasafirishaji wa viumbepori hai nje ya nchi (Tanzania wildlife exporters association-Twea), tunatoa pongezi za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi hiyo.

Mhariri,


Chama cha wasafirishaji wa viumbepori hai nje ya nchi (Tanzania wildlife exporters association-Twea), tunatoa pongezi za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa nafasi hiyo.

Tunamuombea kwa Mungu awe na afya njema na atuongoze kwa hekima na kutuongezea matumaini, amani, umoja na maendeleo.

Tumeona ameanza vizuri kwa kuziangalia wizara, taasisi mtambuka ambazo zinahitaji jicho la tatu kuhakikisha zinaendelea kufanya shughuli zake kwa ufanisi.

Sisi kama taasisi nyingine nasi tuna changamoto nyingi, tunatamani Rais atuangalie ili tuendelee na shughuli zetu kwa ufanisi.

Eneo letu la biashara ya viumbepori hai nalo lliangaliwe upya na Rais wetu kwa jicho la huruma.

Enock Muganyizi, Mwenyekiti, TWEA