Tuipe nafasi afya kwa kupambana na corona, maendeleo yapo tu

Muktasari:

  • Hapo Arusha na Kilimanjaro viongozi wanapoteza sana maisha, huo utalii mnaoutangaza ili kutangaza vivutio kwa wageni wa nje ndio unaopelekea nchi inapata mawimbi ya magonjwa ya ajabu ajabu.

Mhariri,

Hapo Arusha na Kilimanjaro viongozi wanapoteza sana maisha, huo utalii mnaoutangaza ili kutangaza vivutio kwa wageni wa nje ndio unaopelekea nchi inapata mawimbi ya magonjwa ya ajabu ajabu.

Mara mnatangaza utalii, mara mnakopa pesa kuendeleza miradi, mara mnataka katiba mpya, mara mnapanua wigo wa kulipa kodi, mara mnajadiliana na wawekezaji. Kifupi ni kwamba nchi haijakaa kimkakati, inatapatapa kama mfa maji, na bahati mbaya wimbi la tatu la corona likituzidia tutaumia sana.

Nashauri, tupambane kwanza na afya, tukishaimarika basi tutafanya hayo maendeleo. Kwani tukishughulikia ugonjwa ukaisha kisha tukaendelea na masuala ya miradi ya maendeleo mtakuwa mmepoteza nini? Shida washauri wengi wanatumia matumbo badala ya kichwa.

Hallson Mengere