Tutumie nguvu kulinda Katiba na si kuivunja

Wednesday April 28 2021
katiba pc

Hakuna ubishi kuwa uwepo wa wabunge 19 wa viti maalumu waliokuwa wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) una walakini, lakini bado najiuliza kwa nini tunatumia nguvu kubwa kuivunja Katiba kuliko kuilinda?

Nimelazimika kuuliza swali hili baada ya Aprili 23, 2021 kuona mabishano Bungeni kati ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na Mbunge asiye na chama, Jesca Kishoa, ambayo nimeyatafsiri kama ni kulazimisha uvunjifu wa katiba kuliko kuilinda.

Ngoja nikurejeshe kwenye sinema yenyewe, siku hiyo Jesca akichangia mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, alikiri wazi wazi kuwa ameondolewa Chadema.

Haraka haraka Naibu Spika aliingilia kati na kumtaka aifute kauli hiyo kwa sababu ofisi ya Spika haina hiyo taarifa ya kuondolewa kwenye chama chake na kwamba kama angekuwa ameondolewa Chadema, basi asingekuwa ndani ya Bunge. “Kwa sababu wote waliopo humu wana vyama vya siasa na ndio Katiba yetu inavyosema na wewe unaitetea,” alisema Naibu Spika na Jesca akajitetea bado ni mwanachama wa Chadema kwa sababu wamekata rufaa na taratibu zinaendelea.

Hapo Naibu Spika akaingilia tena na kusema taarifa rasmi za Bunge ni kumbukumbu na kumtaka afute sentensi ya kwamba aliondolewa kwenye chama, kwa sababu itakuwa ni kuvunja Katiba kuwa naye kama alishaondolewa Chadema. Naibu Spika akaongeza kusema:

“Na ofisi ya Spika haina taarifa ya wewe kuondolewa uanachama ndio maana uko humu ndani. Futa hiyo kauli tafadhali”, na kauli hii ilikuwa kama amri, hivyo Mbunge Jesca akasema amefuta hiyo kauli.

Advertisement

Nimejaribu kueleza kwa kirefu suala hilo lililojitokeza bungeni, hasa kwa kuwa kwanza Chadema imekana kuwahi kupeleka NEC majina ya wabunge hao 19 na hakuna ubishi kuwa Kamati Kuu ya Chadema ilikutana na kuwafuta uanachama.

Kwanza kabla ya kujadili sintofahamu hizo pengine tujifunze ukuu wa Katiba na Utawala wa Sheria na haya yote yameelezwa katika falsafa nyingi za magwiji wa katiba na sheria duniani na yeyote aliyeapa kuilinda, anawajibika kufanya hivyo.

Ukuu wa Katiba unatamkwa katika kesi maarufu ya India ya Indira Nehru Gandhi dhidi ya Raj Narainya ya mwaka 1976 ambayo pia inapatikana kwenye andiko la Mirza Hameedullah Beg katika ukurasa wake wa 114.

Katika ukurasa huo katika andiko hilo maarufu sana wanasema uhalali wa tendo lolote la serikali au mamlaka lazima liweze kupimwa kwa kuangalia kama linaendana na matakwa ya Katiba, na kwa Tanzania katiba yetu ya 1977.

Wakaendelea kusema: “Usiwepo muhimili wowote, iwe serikali, mahakama au bunge litakalotenda nje ya wigo wa masharti ya Katiba yao”.

Utawala wa sheria unaanzia kwa watawala na ndiyo maana hayati Lord Denning, aliyewahi kuwa Jaji mkuu wa Uingereza alisisitiza sana umuhimu wa watawala kuheshimu utawala wa sheria na kubwa zaidi kuheshimu ukuu wa Katiba.

Katiba yetu imeyaakisi mambo hayo katika ibara ya 13, inayoeleza usawa mbele ya sheria na Ibara ya 34(2) inasema mamlaka ya serikali itakuwa ni kwa ajili ya kutekeleza na kuisimamia Katiba.

Ibara ni nyingi, walau kwa hizo zinaonyesha Katiba yetu inataka wote tufuate utawala wa sheria na ukuu wa Katiba kwa maana lolote linalofanywa lizingatie Katiba ambayo ndio sheria mama.

Tusisahau Spika, viongozi wetu wamekula kiapo cha kuisimamia, kuilinda na kuitetea Katiba, kwa hiyo kama ni watu wa kwanza kuhakikisha Katiba yetu haivunjwi, ni wale waliopa kulinda na kuitetea.

Nimkumbushe Spika na Naibu wake kuwa Ibara ya 72(1)(e) ya katiba aliyoapa inasema mtu atakoma kuwa mbunge kama atakuwa amekoma kuwa mwanachama wa chama alichokuwapo wakati akichaguliwa kuwa mbunge.

Katiba siku zote iko juu ya sheria zote zinazotungwa na ndio maana nasema ukitizama yanayoendelea bungeni na wabunge hao 19 ni kama Bunge ambalo ndio linatunga sheria, linaamua kuweka mfano mbaya wa kuvunja Katiba.

Sasa kama Katiba inasema Mbunge anakoma ubunge akifukuzwa uanachama, na Chadema imewafuta uanachama wabunge hao 19, hivi tunapata ujasiri wapi wa kuendelea kuwaacha bungeni wakilipwa kwa kodi za Watanzania?

Kukata rufaa haifuti uamuzi uliosababisha kukata rufaa mpaka kuwe na uamuzi

Kukata rufaa haifuti uamuzi uliosababisha kukata rufaa mpaka kuwe na uamuzi wa rufaa, kwa hiyo kutumia fedha za umma kuwalipa wabunge hawa ni kinyume cha sheria, lakini pia ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

0769600900

wa rufaa, kwa hiyo kutumia fedha za umma kuwalipa wabunge hawa ni kinyume cha sheria, lakini pia ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

0769600900

Advertisement