Hee! Mbrazili wa Singida atimka

KAMA ambavyo ilikuwa kwa nyota wa England, Raheem Sterling aliyeondoka Qatar kwenye kambi ya timu ya taifa kwenye fainali za Kombe la Dunia ndivyo ilivyokuwa kwa Mbrazil wa Singida BS, Peterson Da Cruz ‘Peu’ ambaye amerejea kwao kutokana na matatizo ya kifamilia.

Peu alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye michezo ya ligi ambayo ameitumikia timu hiyo kuanzia alipojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu akifanikiwa kufunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Prisons.

Kocha wa Singida BS, Hans Van Der Pluijm, alithibitisha kuondoka kwa mshambuliaji huyo na ndiyo maana hakuonekana kwenye michezo kadhaa iliyopita ya Ligi Kuu Bara ukiwemo wa jana, Jumatano dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

“Kuna mambo ya kifamilia ameenda kuyashughulia hivyo uongozi ilimpa baraka zote,” alisema kocha huyo.