Makambo mpya! kumaliza kiburi cha Simba SC

MASHABIKI wa Yanga kwa sasa wanatakiwa watulie tu ili wale raha, kwani zile stresi walizokuwa nazo tangu chama lao lilivyomuuza Heritier Makambo nchini Guinea na kukosa mkali wa kutupia nyavuni zitayeyuka kutokana na mkakati wa mabosi wao kuataka kushusha ‘Makambo’ mpya.

Juzi huko Afrika Kusini, Kigogo wa Yanga, Injinia Hersi Said alikuwa katika kikao kizito cha kupewa straika Lazarous Kambole na taarifa hizo zikamfikia kocha wa Zesco United inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia, aliyetamka kwamba sasa Yanga itakuwa imepata mtu wa maana.

Hersi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano jana alikuwa katika kikao na mabosi wa Kaizer Chiefs, Bobby Kaizer katika kupewa kwa mkopo Kambole ambaye ameshindwa kuingia katika kikosi chao cha kwanza.

Mchakato huo, ukamuibua Kocha Msaidizi wa Zesco, iliyobakisha pointi mbili tu ili kuwa bingwa nchini Zambia, Noel Mwandila aliyeliambia Mwanaspoti kwamba tangu kuondoka kwa Makambo kwa sasa Yanga ndio itakuwa inamshusha straika wa kati anayejua kufunga.

Makambo aliyeichezea Yanga kwa msimu mmoja na kufunga mabao 17 katika Ligi Kuu Bara akishika nafasi ya tatu nyuma ya kinara Meddie Kagere aliyemaliza na 23 na Salim Aiyee aliyekuwa Mwadui aliyefunga mabao 18.

Tangu kuondoka kwake Jangwani kwenda kujiunga na AC Horoya, Yanga ilikuwa haijapata straika wa maana wa kufunga lichja ya kuwaleta kina David Molinga, Yikpe Gnamien, Juma Balinya na msimu huu kubeba kina Fiston Abdulrazaq, Saido Ntibazonikiza na wengine, ambao hata huivyo wameshindwa kufikia moto aliokuwa nao Mkongamani huyo, yaani Makambo.

Akizungumza na Mwanaspoti kutoka Zambia, Mwandila aliyewahi kuinoa Yanga akimsaidia George Lwandamina aliyepo sasa Azam FC, alisema; “Namjua Kambole ni mshambuliaji ambaye amekamilika nafikiri tangu kuondoka kwa Makambo (Heritier) sasa ndio kuna mshambuliaji wa maana wanaweza kuwa wamempata,” alisema Mwandila aliyewahi kukaimu ukocha mkuu Yanga.

“Kambole atacheza Yanga na atawasaidia sana, anajua kufunga ana kasi lakini pia ni mshindani sana,kuna kiongozi wa Yanga alinipigia (anamtaja ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji) pia kuuliza kama atawafaa nimemjibu kwamba ni uamuzi sahihi,” aliongeza.

Kocha huyo alisema, Kaizer Chiefs walikuwa wanakosea jinsi ya kumtumia Kambole na hata ligi ya Sauzi ni kubwa na ina ushindani.

“Kambole alifanya vizuri sana alivyokuwa hapa Zesco alikuwa anafunga mpaka mabao 20 kwa uchache Kaizer walikuwa wanamchezesha kama winga nafasi ambayo kama unataka kuona makali ya Kambole hilo halikuwa eneo sahihi. Nimewaambia eneo sahihi la Kambole wamchezeshe katikati watafurahia usajili huu. Naijua Ligi ya Tanzania kwa mabeki wa hapo itakuwa ngumu kumzuia kwa kuwa naye ni mpiganaji.