Afrika Super League rasmi Agosti 2023

Muktasari:

  • Mashindano ya Afrika Super League ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na wadau wengi yamezinduliwa jijini Arusha huku yakipangwa kufanyika Agosti 2023.

Mashindano ya Afrika Super League ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu na wadau wengi yamezinduliwa jijini Arusha huku yakipangwa kufanyika Agosti 2023.

Mashindano yatashirikisha timu 23 kutoka kanda zote sita huku kila kanda itatoa timu tatu ambazo zitapata fedha za maandalizi Dola 3.5milioni.

Mbali na hapo zawadi kwa mshindi wa kwanza itakuwa ni Dola 11.5 milioni ambapo Rais wa CAF, Patrice Motsepe amesema mipango yao ni kuhakikisha Soka la Afrika inakuwa na ushindani sawa na mabara mengine.

Amesema soka la Afrika lazima likue na ushindani mkubwa kama ilivyo kwa wengine ambapo kama uongozi lazima watalipambania na kulifanikisha hilo.

Afrika Super League rasmi Agosti 2023

Mtendaji mkuu wa Simba, Barbara Gonzales anasema kama Mtanzania anajivunia miongoni mwa watu ambao walihudhuria mkutano huo ambapo ni jambo la kipekee kwanza kushuudia pia uzinduzi wa Afrika Super League.

Anasema ni heshima kuwa na Rais wa FIFA kwani anapofika Tanzania anafanya uchunguzi kwanza kuna nini Tanzania nini inaendelea kwenye Mpira Kimataifa ambapo itakuwa jambo jema ambayo kwake anaamini ni fursa kwa soka letu.

Mkutano huo  unahusisha wajumbe 156  kutoka nchi 52 wanachama CAF kati ya nchi 154 huku Kenya na Zimbabwe hazijashiriki mkutano huo kutokana na kufungiwa na FIFA.

Mkutano huo pia umehudhuriwa na zaidi wa watu 400 kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais wa FIFA, Gianni Infantino, Rais wa Soka Qatar (QFA), Sheikh Ahmad Thani,waziri mkuu Kassim Majaliwa wengine.