Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arusha yaendeleza makali kikapu Umitashumta 2025

Timu wa Wanafunzi wa shule za msingi Arusha wakiwa viwanja vya Kichangani halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakiteta jambo na walimu wao baada ya mchezo dhidi ya Mtwara. Picha na Christina Thobias

Muktasari:

  • Ubavu wa timu ya Wanawake Arusha kwenye kikapu umeoneshwa leo Juni 11 baada ya kuitwanga Tabora 27-7 huku jana Juni 10, 2025 Arusha ikiwakanda Mtwara 50-3 katika mechi yao iliyochezwa jioni katika viwanja vya Kichangani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

‎Iringa. Viwanja vya Kichangani vilivyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa vimeendelea kuwaka moto kwa michezo ya kusisimua ya mpira wa kikapu (basketball), huku timu ya Arusha ikiendeleza ubabe wake kwenye mashindano hayo.

‎Katika michezo ya leo Juni 11, 2025 kwa upande wa Wanawake, Mwananchi Digital imeshuhudia timu ya Arusha ikionyesha kiwango cha juu kwa kuicharaza Tabora kwa pointi 27-7, na kuonyesha kuwa bado ni moto wa kuotea mbali katika mashindano haya ya kitaifa.

‎Mchezo mwingine ulioshuhudiwa leo ulikuwa kati ya Iringa na Mbeya, ambapo Mbeya waliibuka kidedea kwa ushindi wa pointi 22-2 dhidi ya wenyeji Iringa ambapo mchezo huo ulikuwa na mvuto wa kipekee, lakini Mbeya walionyesha nidhamu ya hali ya juu na umakini wa kupigiwa mfano.

‎Katika mtanange mwingine, Mwanza waliifunga Tanga kwa pointi 22-1, huku wakionesha kuja kivingine mwaka huu wakiwa na safu bora ya ushambuliaji.

‎Nao Singida waliibuka na ushindi mwembamba wa pointi 9-7 dhidi ya Rukwa, katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa hadi dakika za mwisho.

‎Pwani nao waliweka rekodi kwa kuwachapa Manyara kwa pointi 16-9, wakionekana kuja kwa kasi kwenye mashindano haya. Kagera waliendelea kutoa somo kwa Katavi kwa kuibuka na ushindi wa pointi 18-5, wakionyesha kuwa ni miongoni mwa timu zinazopaswa kuchungwa.

‎Kwa upande wa timu za UMITASHUMTA zilizoshiriki mchezo wa kikapu jana matokeo yalikuwa hivi,

‎Kwa upande wa wasichana, jana michezo 11 ilipigwa katika viwanja hivyo hivyo vya Kichangani, ambapo Arusha waliweka historia kwa kuibuka na ushindi mkubwa zaidi wa mashindano haya kwa kuwachakaza Mtwara kwa pointi 50-3, ushindi unaodhihirisha kuwa wao si wa kubezwa.

‎Katika mchezo wa kwanza, Mwanza waliicharaza Kilimanjaro kwa pointi 26-7, chini ya uchezeshaji wa Mark Hassan (crew chief), Msuka Godlisten na Yohana Mwenge.

‎Mchezo wa pili ulishuhudia Mbeya wakiibuka na ushindi wa pointi 11-7 dhidi ya Shinyanga, ukiendeshwa na waamuzi Sweetbert, Shinda Vincent, na Benjamin Wilfred.

‎Katika mchezo wa tatu, Arusha waliendelea kuporomosha mvua ya vikapu kwa kuibuka na ushindi wa pointi 43-6 dhidi ya Singida, huku wakichezeshwa na Witness Mwera , Shinda Vincent , na Patrick Semindu .

‎Geita waliibuka kidedea kwa ushindi wa pointi 20-16 dhidi ya Ruvuma katika mchezo wa nne, ukichezeshwa na Mark Hassan , Witness Mwera , na Yohana Mwenge .

‎Dodoma waliwazidi maarifa Katavi kwa pointi 13-5, mchezo wa tano ambao ulichezeshwa na Elvis Kabera, Patrick Semindu, na Jima Faraja.

‎Katika mchezo wa sita, Songwe waliwaduwaza Mtwara kwa ushindi wa pointi 20-6, wakichezeshwa na Justine Tija, Esther Simbo, na Jima Faraja.

‎Rukwa waliambulia kichapo cha pointi 14-2 kutoka kwa Tabora katika mchezo wa saba, ukisimamiwa na Benjamin Wilfred, Esther Simbo, na Msuka Godlisten.

‎Mchezo wa nane kati ya Kagera na Tanga ulisimamiwa na Justin Tija, Yohana Mwenge, na Msuka Godlisten, huku matokeo yakisubiriwa kutokana na utata wa baadhi ya takwimu.

‎Katika mchezo wa tisa, Ruvuma waliwafunga Pwani kwa pointi 10-6, ukichezeshwa na Patrick Semindu, Benjamin Wilfred, na Amir Juma.

‎Mchezo wa kumi ulishuhudia Shinyanga wakiichapa Dar es Salaam kwa pointi 8-4, ukisimamiwa na Shinda Vincent, Mark Hassan, na Elvis Kabera.

‎Hatimaye, mchezo wa kumi na moja ambao ulikuwa gumzo la jiji, Arusha waliwaadhibu Mtwara kwa pointi 50-3 ambapo mchezo huo ulichezeshwa na Msuka Godlisten, Witness Mwera, na Sweetbert Magoti, na kuacha mashabiki wakishangilia kwa nguvu mafanikio ya mabingwa hao watetezi.

‎Aidha mashindano hayo yanayoendelea Iringa yameendelea kuonyesha ukuaji mkubwa wa mchezo wa kikapu nchini huku timu ya Arusha imeendelea kutikisa viwanja kwa ubora wa hali ya juu, pia waamuzi mbalimbali wakisifiwa kwa kusimamia mechi kwa weledi mkubwa.

‎Mashindano yanaendelea kesho kwa michezo zaidi, huku wadau wa michezo wakiendelea kujitokeza kwa wingi kushuhudia vipaji vipya na ushindani wa hali ya juu kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.