Aziz Ki atua Dar kuiwahi Al Hilal

Aziz Ki awawahi Al Hilal

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameingia nchini rasmi tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo itakayoanza kesho kwa maandalizi ya kuikabili Al Hilal ya Sudan kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki ameingia nchini rasmi tayari kujiunga na kambi ya timu hiyo itakayoanza kesho kwa maandalizi ya kuikabili Al Hilal ya Sudan kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Aziz Ki alikwama nchini Morocco kufuatia kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 akiwa katika vipimo vya mwisho kuondoka nchini humo alipokwenda kuitumikia katika michezo miwili ya kirafiki iliyokuwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Baada ya kuzuiliwa kwa siku kadhaa nchini humo mshambuliaji huyo alikuja kufanyiwa tena vipimo ili kuangalia maendeleo yake na vipimo kuonyesha hana maambukizi ndipo aliporuhusiwa na mamlaka hiyo.

Yanga inarudi mazoezini kesho huku ikieleza kuwa Aziz Ki atakuwa mmoja wa wachezaji watakaoingia kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan baada ya kuonekana yuko fiti licha ya matokeo ya vipimo hivyo.

Yanga itakuwa Uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa Oktoba 8, 2022 kuwakaribisha Al Hilal katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kurejea kwa Aziz Ki Kutawashusha presha mashabiki wa Yanga ambao waliingia na wasiwasi katika kumkosa mshambuliaji huyo katika mechi hiyo muhimu.