Bao la Carlinhos lamuokoa Kaze

Bao la Carlinhos lamuokoa Kaze

Muktasari:

  • HIVI uliona namna Kocha Cedric Kaze alivyoshangilia kwa nguvu bao la Carlinhos dhidi ya Mtibwa Sugar? Sasa wazee wa chini chini wanadai, ilikuwa lazima Kaze ashangilie bao lile kuliko hata alivyoshangilia mfungaji kutokana na ukweli alikuwa kwenye hali mbaya.

HIVI uliona namna Kocha Cedric Kaze alivyoshangilia kwa nguvu bao la Carlinhos dhidi ya Mtibwa Sugar? Sasa wazee wa chini chini wanadai, ilikuwa lazima Kaze ashangilie bao lile kuliko hata alivyoshangilia mfungaji kutokana na ukweli alikuwa kwenye hali mbaya.

Inadaiwa kocha huyo alikuwa katika wakati mgumu baada ya kupata matokeo ambayo yalikuwa hayawafurahishi mabosi wa klabu hiyo.

Kaze aliwekwa mtu kati na kuambiwa yupo katika wakati mgumu kama timu hiyo haitapata ushindi tena.

Alipopata ushindi katika mchezo dhidi ya Mtibwa, kocha huyo alishindwa kabisa kuficha hisia zake kwani alishangilia vilivyo na kuruka ruka.

Licha ya kupata ushindi bado Kaze alizua maswali ya kwanini alimweka nje Carlinhos muda mrefu kwani kila akiingia amekuwa na matokeo chanya.

Imeandikwa na

THOMAS NG’ITU