Betika yaja na Twende Kibingwa, yajikita kwenye Ligi kubwa duniani

Thursday August 11 2022
bet pic
By Imani Makongoro

Kampuni ya michezo ya kubashiri matokeo ya Betika imepanua wigo kwa Watanzania kuvuna pesa katika mchezo wa kubashiriki matokeo ya mechi za Ligi kubwa za soka duniani kwenye Kitonga Jackpoti.

Zawadi Gabriel, Meneja mauzo wa Betika amesema Kitonga Jackpoti inashirikisha utabiri kwenye mechi za EPL, La Liga, UEFA, Seria A na Ligi kuu ya Tanzania sanjari na michezo mingine ikiwamo ya Cassino.

"Kwa kuanzia washindi watavuna hadi Sh251 milioni, na itakuwa ikiongezeka kila wiki," amesema Zawadi leo katika uzinduzi wa Jackpoti hiyo iliyokuwa na kauli mbiu ya Twende Kibingwa uliofanyika jijini Dar es Salaam.

bet pic 1

Amesema kwenye Kitonga Jackpoti ni rahisi kubadili maisha kwa kuwa milionea au bilionea kwa Sh 2000 ambayo inatoa fursa ya kuvuna hadi Sh251 milioni.

Meneja bidhaa wa Betika, Samwel Lawrence amesema, katika Kitonga Jackpoti unaweka ubashiri kwenye mechi 13 na inatoa mamilioni ya pesa kwa washindi.

Advertisement

"Si wakati wa kukaa kinyongo, Twende Kibingwa Kitonga Jackpoti inakupa fursa ya kubadili maisha na kukupa nafasi ya kuwa milionea, hii si ya kukosa.

"Pia kuna Dabo Chance ambayo ambayo inakupa nafasi tano za kuchagua timu ipi uipe ushindi au uipe matokeo ya sare.

"Hii inatoa nafasi ya kuchagua timu fulani ipate sare au ishinde, lakini pia kuna Kijumbe Quick ambayo inakurahisishia kazi ya kubet," amesema Samwel.

Amesema kuna nafasi tatu za kuwa mshindi kwenye Jackpoti moja katika promosheni hiyo ambayo imezinduliwa leo na itakuwa ikitoa mshindi mmoja kila wiki.

Aliyewahi kuwa msemaji wa Yanga, Anthonio Nugaz amesema Jackpoti hiyo haijawahi kutokea nchini.

"Mechi 13 tu unashinda kwa buku mbili (Sh2,000), lazima Dar es Salaam na Tanzania watambe ni fursa kwa wale wenye bahati kubadili maisha," amesema

Advertisement