'Certified Lover Boy' ya Drake yaweka rekodi ya mauzo

Friday September 10 2021
DREAKPICC
By Peter Akaro

Rapa kutoka Marekani, Drake ameendelea kufanya vizuri na albamu yake mpya 'Certified Lover Boy' ambayo sasa imefanikiwa kufikisha mauzo ya nakala 500,000 (Gold)  ndani ya kipindi cha wiki moja na kuweka rekodi.

Albamu hiyo yenye nyimbo 21 na muda wa saa moja na dakika 22, ilitoka rasmi  Septemba 3, 2021 chini ya lebo ya Republic OVO Sound ikiwa ni ya sita kwa Drake tangu aanze muziki.

Kwa mujibu wa RIAA (Recording Industry Association of America), Certified Lover Boy ndio albamu ya kwanza kwa mwaka huu kufikia mauzo ya Gold kwa kipindi hicho.

Juni 15, 2010 Drake alitoa albamu yake ya kwanza 'Thank Me Later' chini ya Yong Money & Cash Money pamoja na Universal Motown Records, kisha zikafuata nyingine kama ‘Take Care’ (2011), ‘Nothing Was The Same’ (2013), ‘Views’ (2016) na  ‘Scorpion’ (2018).

Advertisement