'Nomadland' yapata ushindi mkubwa tuzo za Oscars

Tuesday April 27 2021
oscar pc 2
By AFP

Hollywood, Marekani (AFP). Sinema ya barabarani ya "Nomadland" jana Jumapili imepata ushindi mkubwa katika tamasha la kutuza wacheza filamu la Oscars, ikitwaa tuzo tatu kubwa ikiwemo ya muongozaji Chloe Zhao.

Tamasha hilo limefanyika wakati Hollywood ikisherehekea moja ya siku muhimu kwa staili ya aina yake kutokana na janga la virusi vya corona.

Filamu ya mtukio ya kusisimua ya Zhao kuhusu Wamarekani wanaokandamizwa wakizurura Magharini kwa malori, ilishinda tuzo ya Picha Bora, Muongozaji Bora na Muigizaji Bora wa Kike kutokana na ustadi wa Frances McDormand, ambaye sasa ameingia katika orodha ya magwiji baada ya kutwa atuzo ya tatu ya Oscars.

Anthony Hopkins, ambaye hakuibuka katika tamasha hilo, alishangaza watu alipoibuka na tuzo ya Muigizaji Bora, ambayo ilikuwa ya mwisho usiku wa jana, akimbwaga Chadwick Boseman, aliyekuwa akipewa nafasi kubwa na ambaye alifariki mwaka jana kutokana na saratani.

Tamasha hilo lilihamishwa kutoka ukumbi wa sinema wa Hollywood hadi katika kituo cha treni kuheshimu masharti ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, na kukutanisha kwa mara ya kwanza wasanii nyota wa Tinseltown katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Zhao, ambaye ni mwanamke wa kwanza asiye mweupe kuwahi kushinda tuzo ya Mwongozaji Bora, alishukuru "watu wote tuliokutana nao barabarani... kwa kutufundisha nguvu ya uthabiti na matumaini, na kutukumbusha ufadhili ukoje."

Advertisement

Pia amekuwa mwanamke wa pili kushinda tuzo ya Mwongozaji Bora baada ya Kathryn Bigelow, ambaye alivunja mwiko mwaka 2010 aliposhinda tuzo hiyo kutokana na filamu yake ya "The Hurt Locker."

"Inafurahisha kuwa mwanamke mwaka 2021," Zhao aliwaambia waandishi wa habari katika mahojiano nyuma ya jukwaa, akiongeza: "Kama ushindi huu unamaanisha watu zaidi wanaishi ndoto zao, ninashukuru kupita kiasi."


Huku majumba ya sinema yakiwa yamefungwa kwa mwaka mzima, filamu ya Zhao, ambaye ni mzaliwa wa Beijing, alionyesha sakata la corona kwa kutumia taswira za watu waliotengwa katika jamii.

"Tafadhali angalia sinema yako katika mtazamo mkubwa kadri uwezavyo. Na siku moja, karibu sana, mpeleke kila unayemjua katika jumba la sinema, bega kwa bega katika sehemu hizo ya giza, na angalia kila filamu inayoonyeshwa usiku wa leo," alisema McDormand.

oscar pc 3

Zhao, ambaye amesababisha utata nchini China baada ya kuonekana akiikosoa nchi yake katika mahojiano, pia alikariri shairi la zamani la Kichina katika hotuba yake ya shukrani.

Ushindi wa Hopkins, ambaye ana miaka 83, unaotokana na jinsi alivyoigiza kama mtu mwenye matatizo ya akili katika filamu ya "The Father", unamfanya kuwa mwigizaji mwenye umri mkubwa kushinda tuzo yenye ushindani katika historia ya Oscar.

Lakini hakusafiri kwenda Los Angeles au London kushukuru kupokea tuzo, na ushindi wake bila ya hotuba ya shukrani, ulifanya siku ya jana iishe kiajabu.

Tuzo ya Muigizaji Bora Msaidizi ilikwenda kwa Youn Yuh-jung kutokana na uigizaji wake katika filamu ya mhamiaji wa Kikorea ya "Minari."

"Nawezaje kumshinda Glenn Close?" alisema, akimzungumzia mshindani mwenzake katika kipengele hicho ambaye alitajwa kuwania tuzo nane lakini aliondoka mikono mitupu.

Daniel Kaluuya alishinda tuzo ya Mwigizaji Bora Msaidizi wa Kiume kwa jinsi alivyomuigiza kiongozi wa Black Panthers katika miaka ya sitini, Fred Hampton katika filamu ya "Judas and the Black Messiah," ambayo pia ilishinda tuzo ya Wimbo Bora ulioimbwa na H.E.R, ambaye ametwaa tuzo kadhaa za muziki za Grammy

Advertisement