Album ya DMX yakamilika siku 48 baada ya kifo chake

Friday May 28 2021
dmaxpic
By Mwandishi Wetu

New York, Marekani (AFP). Nyota wa rap, DMX alikuwa amepania kurejea kwa nguvu katika muziki kabla ya kifo chake kilichostua, na sasa albamu yake iko tayari kwa ajili ya kuachiwa leo Ijumaa Mei 28, 2021 baada ya miaka kumi.

Lakini, rapa huyo aliyefariki akiwa na miaka 50 alitamba katika miaka ya tisini na mwanzoni mwa milenia hii akiwa na albamu tano zilizoshika nafasi ya juu katika chati za nyimbo baada ya kuzinduliwa, hajaweza kuona albamu yake mpya ya "EXODUS" ikiingia sokoni ikiwa imetayarishwa na Def Jam Recordings.

Kuna hisia za ukombozi katika albamu hiyo yenye nyimbo 13, mada ambayo inagusa hisia baada ya kifo cha msanii huyo.

Alifariki Aprili 9 akiwa hospitalini ambako aliwekewa mashine ya kumsaidia kuendelea kuishi kwa karibu wiki moja baada ya kupata shambulio la moyo.

Albamu yake rasmi ya nane inawashirikisha kwa kiasi kidogo wasanii nyota wa juu yake, akiwemo Jay-Z, Nas na Snoop Dogg, huku ikiwoanyesha Alicia Keys, Usher na Bono.

Alama ya DMX ya rapa aliyeibukia New York, inaonekana katika baadhi ya nyimbo, zikiwemo "That's My Dog," "Hood Blues" na "Bath Salts".

Advertisement

Lakini pia ustadi wake mwingine kama wa mashairi na anayejali pia unaonekana katika wimbo wa "Hold Me Down". Katika wimbo wa "Letter to My Son" baba huyo watoto 15 anaonyesha machungu ya ndani na maisha ya kuchanganyikiwa kwa kutumia lundo la violin.

Rafiki wake wa muda mrefu na mtayarishaji muziki, Swizz Beatz, ambaye jina lake halisi ni Earl Simmons, aliongoza kukamilisha albamu ya "EXODUS" to completion.

"Kaka yangu X alikuwa mmoja wa watu adimu wakweli na wenye roho nzuri ambao nimewahi kukutana nao. Maisha yake yalijielekeza kwa familia yake na muziki," alisema Swizz Beatz kabla ya albamu hiyo kutolewa.

"Zaidi ya yote alikuwa mwema kutokana na utoaji na aliwapenda mashabiki wake kupita kiasi."

Advertisement