Angella apata tuzo ya kwanza, ashindwa kuifikia rekodi ya Zuchu

Monday June 07 2021
Angela pc
By Mwandishi Wetu

Hatimaye msanii wa Bongofleva kutoka Konde Music Worldwide, Angella amefanikiwa kupata tuzo ya kwanza kutoka chaneli yake kufikisha wafutiliaji (subscribers) 100,000.

Angella ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo 'Nobody' amefikia mafanikio hayo ikiwa ni miezi mitatu tangu atangazwe rasmi kuwa chini ya lebo hiyo inayomilikiwa na Harmonize. Baada ya kusaini mkataba aliachia wimbo wake wa kwanza uitwao ‘Kama’ aliomshirikisha  Harmonize ukiwa ni wa pili kufanya pamoja.

Katika kuwashukuru mashabiki wake, Angella amesema

"Haikuwa kazi rahisi toka nimeianza safari yangu ya muziki rasmi, nimeuona upendo wenu wa dhati mashabiki zangu ambao mmejitolea muda wenu kufuatilia kazi zangu.


Angella wa Konde Music, anayewekwa  kwenye mizani na Zuchu wa WCB kutokana na historia ya kuanzishwa kwa lebo hizo, amechukua muda mrefu zaidi kupata wafuasi 100,000 ukilinganisha na mwenzake.

Advertisement


Zuchu ilimchukua wiki moja pekee kufikisha wafuasi 100,000 kwenye mtandao wa YouTube na kuweka rekodi ya kuwa  msanii wa kwanza wa kike Afrika kufanya hivyo, kisha naye akapata Silver Button Award. Baadaye akaja kushinda tuzo ya African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) kipengele cha msanii bora chipukia. 


Kufikia Machi 26 mwaka huu,  Zuchu alifanikiwa kufikisha wafuasi milioni moja  na kuwa msanii wa kwanza wa kike Tanzania na Afrika Mashariki kufanya hivyo. Kwa ujumla anakuwa msanii wa tano Tanzania kufikia rekodi hiyo baada ya Diamond, Harmonize, Rayvanny na Mbosso. 

Wasanii wa kike watano Bongo wenye wafuasi  wengi Youtube;


1. Zuchu - milioni 1.21

2. Nandy - 775,000

3. Vanessa Mdee - 281,000

4. Maua Sama - 251,000

5. Hamisa Mobetto - 128,000

Advertisement