Audiomack yazindua kampeni kuupaisha muziki wa Kitanzania

Muktasari:
- Kampuni ya Audiomack imezindua kampeni inayojulikana “Ngoma Juu Ya Ngoma” inayolenga kukuza ubunifu na kuuza muziki wa Kitanzania.
Dar es Salaam. Kampuni ya Audiomack imezindua kampeni inayojulikana “Ngoma Juu Ya Ngoma” inayolenga kukuza ubunifu na kuuza muziki wa Kitanzania.
Kampeni hiyo itashirikisha wasanii wakubwa wakiwemo Zuchu, Lava Lava, Jux, Barnaba na wengine ambapo itahusisha Bango, ushirikiano wa Radio na matangazo ya kidijitali, chapa ya mabasi, ushiriki wa watu wenye ushawishi na orodha za kucheza.
Katika kukuza uelewa juu ya kampeni hiyo, Audiomack ilifanya Warsha hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Audimack, Jason Johnson, alisema kampeni hiyo itahusisha mabango, redio na matangazo ya kidigitali, matangazo kwenye mabasi, ushiriki wa watu wenye ushawishi.
Pia, alisema kampeni hiyo itahusisha wamuziki mbalimbali wa kimataifa wa Audiomack, SKYLINE, na maonesho yanayohusisha tamaduni kutoka Tanzania na kuziweka katika ubora wa juu zaidi.
Alisema Audiomack pia imeshirikiana na kituo cha redio Wasafi FM kilichoshinda tuzo za kuzindua Audiomack Top 10.
“Kipindi hicho kinachorushwa Ijumaa, kinaundwa na chati za Audiomack Top 10 Tanzania zinazoangazia nyimbo kubwa zaidi chini,” alisema.