Baba Levo ahojiwa Basata kwa saa mbili

Thursday April 15 2021
By Nasra Abdallah

Dar es Salaam. Msanii wa Bongofleva, Clayton Chipando maarufu baba Levo amehojiwa na Baraza la Sanaa  la Taifa (Basata) kwa saa mbili.


Hata hivyo, Basata na Baba Levo  hawakueleza msingi wa mahojiano hayo lakini msanii huyo alipewa wito huo na kutakiwa kufika leo Alhamisi Aprili 15, 2021.


Wakati akiondoka katika ofisi za baraza hilo zilizopo Ilala jijini Dar es Salaa, msanii huyo amesema anaelekea polisi anakotakiwa kwenda kutoa maelezo ya suala jingine.


Advertisement

Baba Levo aliwasili Basata saa 4:30  asubuhi na kumaliza saa 6:30 mchana.


Akizungumza baada ya kuhojiwa amesema, “jamani waandishi sipo tayari kuzungumza chochote tulichoongea na Basata katika kikao hicho, labda nendeni mkawaulize wenyewe.”


" Ninachoweza kusema ni kwamba nimeitikia wito wao nimewasikiliza walichoniambia, tumezungumza mengi na  nimemalizana nao na sasa naelekea kituo cha polisi kati nao wameniita.”


Advertisement