Baba wa Nick Minaj afariki dunia

Monday February 15 2021
Nick pic

Robert Miraj ambaye ni baba wa msanii wa Marekani Nicki Minaj, afariki dunia.
Miraj ambaye alikuwa na miaka 64 amefariki dunia alipokuwa hospitalini akipatiwa matibabu, huku chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni ajali ya gari.
Taarifa iliyotolewa na polisi imesema, baba huyo  aligongwa na gari alipokuwa akitembea kando ya barabara huko Long Island Newyork nchini Marekani Ijumaa majira ya jioni, na alifariki dunia siku ya jumamosi.
Hata hivyo jeshi polisi limesema  jitihada za kumtafuta dereva wa gari lililomgonga zinaendelea kwani baada ya tukio alikimbia.
Pia mwakilishi wa Minaj alithibitisha kifo hicho kwa mtandao wa habari wa TMZ, ingawa Nick Minaj mwenyewe hajatoa taarifa yoyote kwa umma juu ya kifo cha baba yake huyo.
Nick Minaji ambaye jina lake halisi Onika Tanya Maraj, anapata msiba huo mzito ikiwa imepita miezi minne tangu alipojifungua mtoto wake wa kwanza, aliyezaa na mumewe Kenneth Petty waliyefunga naye ndoa mwaka 2019.

Advertisement